Katika taarifa siku ya ijumaa ,Owalo amesema ‘muda ulifika kwake kuacha nafasi katika chama hicho’
"... Kukiwezesha ANC kujitayarisha vilivyo na kw amazngira yafaayo kuendelea mbele bila kujibana kutokana na msimamo na maoni yake’
Pia amesema ameichukua hatua hiyo ili kuunda nafasi ya kuzidi kuwepo urafiki wake binafsi na kiongozi wa chama hicho Musalia Mudavadi na uhusiano wao kitaaluma na mzuri ambao umekuwepo kwa miaka zaidi ya 25.
Kujiondoa kwa Owalo kunajiri siku moja tu baada ya Barrack Muluka pia kujizulu kama katibu mkuu wa chama hicho ili kukiwezesha kuwa na mwanzo mpya kablka ya uchaguzi mkuu wa 2022 .
Muluka alisema kujiuzulu kwake kutampa Mudavadi Fursa ya kujifanyia maamuzi yake ya kisiasa kabla ya uchaguzi wa 2022.