Mshukiwa aliyetambuliwa kama Abraham Kipsosion Kibor, anadaiwa kuondoka sehemu yake ya kazi saa kumi na moja jioni ili kumtembelea mpenzi wake katika nyumba ya kukosi bila kumpa notisi kwamba anakuja na alitamaushwa kufungua mlango na kupata akiwa na mwanamme mwingine ambaye sasa ni marehemu Michael Kipyegon mwenye umri wa miaka 36 .
Polisi katika kituo cha Eming waliothibitisha mauaji hayo wamesema mshukiwa baadaye alijisalimisha kwa polisi na pia alimdung kisu mpenzi wake baada ya kumuua jama aliyekuwa akifanya mapenzi naye .
Polisi waliwakimbiza wawili hao katika hospitali moja huko Eldama Ravine lakini mwanamme aliaga dunia kwa ajili ya majeraha aliopata kifuani . mwanamke naye yupo katika hali nzuri baada ya kutibiwa . kisu kilichotumiwa kimehifadhiwa na polisi ili kutumiwa kama ushahidi huku uchunguzi ukianzishwa .