'Buda usiwahi posti picha yangu mbovu kama hio tena,'Octopizzo amwambia King Kaka baaday ya kuposti picha hii

Rappa Henry Ohanga almaarufu Octopizzo amemuonya rappa mwenzake King Kaka dhidi ya kupakia picha za zamani kwenye mitandao ya kijamii iwapo yuko katika picha hizo.

Kwenye mitandao ya kijamii Kaka aliposti picha ya zama wakiwa na rappa Octopizzo na Khaligraph Jones na kuandika ujumbe mfupi, baada ya kuona picha hiyo Octopizzo alimwambia Kaka kuwa picha hiyo haina ubora wowote na ni wa chini.

“@khaligraph_jones @octopizzo waseee manze tumeGrind sana ndio tufike hapa , let’s not loose sight of the journey. Nothing but love." Kaka Aliandika.

Kwa majibu ya haraka Octopizzo hakulaza damu bali alimuonya Kaka dhidi ya kuposti picha kama hiyo kwenye mitandao huku akidai ana picha nyingi sana zenye ubora mwema.

“Buda niko na picha nyingi sana safi safi, usiwai post picha yangu Mbovu kama hio tena.Unafanya drip yangu ifanane na yenyu. That Drip is expensive my friend”.

https://twitter.com/RabbitTheKing/status/1300331318895673344

Kaka naye alimjibu na kumwambia kama hataki picha yake ya kitambo kupakiwa kwenye mitandao ya kijamii wanapaswa kukutana watatu hao na kupigwa picha zenye ubora.

“Hahahahaha unakuwanga na mambo. Basi tutakutana tupige mpya ndio mkiBeef nipost.”

Haya yanajiri siku chche baada ya rappa Octopizzo na khaligraph Jones kuzua ugomvi na cheche za maneno kwenye mitandao ya kijamii baada ya Jones kudai kuwa Octopizzo amenunua mashabiki wake kwenye mtandao wa youtube.