'Ninapo hesabu baraka zangu nakuhesabu,'Ujumbe wa Akothee kwa Baby daddy wake

Msanii Akothee hana uoga wowote wa kumsifu baby addy wake kwa kuwa naye kila wakati, tangu alipokuwa dereva wa texi mpaka mahali alipo sasa kama msanii mkubwa na mwenye kufahamika Afrika Mashariki.

Kupitia kwenye ujumbe wake aliouandika kwenye ukurasa wake wa instagram mama huyo wa watoto tano alifichua kuwa siku kama hii ndio Papa Oyoo alimpendekeza kwake na kumnunullia nyumba yao ya kwanza.

Huu hapa ujumbe wake;

njoo uone msichana uliyepatana naye akiwa dereva wa texi anaishi Shanzu amekuwa staa mkubwa na mwanabiashara."

Akimwandikia na kumtakia siku njema ya kuzaliwa alikuwa na haya ya kumwambia.

"Ulipendwa na wengi na kuheshimiwa na wote, kutoka chini hadi juu, mwanamume ambaye alipenda kuniona nikikua ninapohesabu baraka zangu nakuhesabu mara saba

wewe ni shujaa wangu asante kwa kuwa hapa kwa ajili yangu na watoto,sitasahau safari nyingi ulinipeleka katika mahakama ya watoto kupigania mtoto ambaye si wako Dominic wewe ni nani tena? Help me wish Papa OYOO HAPPY BIRTHDAY."