Atwoli amshambulia DP Ruto asema Naibu wa rais sio ‘Hasla’

atwoli
atwoli
Katibu mkuu wa muungano wa COTU  Franci Atwoli amemshambambulia naibu wa rais William Ruto akisema kwamba Ruto sio hasla . Atwoli amesema Ruto hutoa kiasi kidogo sana cha fedha kwa wananchi ilhali   yeye ni tajiri .

" Unajiita hasla ilahli wewe sio hasla ..kisha unakwenda kanisani  na kusema wongo … tafuta kwenye google ujue hasla ni nani .. ni mtu anaetumiwa njia za  kilaghai kupata pesa…’  Atwoli amesema

" ukiendelea Zaidi utagunmdua kwamba hasla ni kahaba wa kiume ..mbona unataka kujihusisha na jina kama hilo…?’

Atwoli amesema vuguvugu la hasla  ni njama ya kuwalagjai watu maskini nchini akiongeza kwamba Ruto ni mtu tajiri .

" ana ndege tano  ,jumba kubwa  na ardhi kubwa nchini ilhali najiita mtumaskini … wheelbarrows anazopeana ni vitu vidogo sana ukilinganisha na mali yake ,hatuwezi kuunda serikali ya watu wanaocheza kamari’ amesema Atwoli

" Hatutawaruhusu watoto wetu kujiita hasla na tunapigania kuundwa kwa seriokali nzuri ya kuleta mazingira mema kwa kila mkenya .

Wakati huo huo Atwoli amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuwafuta kazi mawaziri wote wanaokosa kushughulikia masuala ya wafanyikazi

" Mawaziri  ambao hawatilii maanani maslahi ya wafanyikazi hawaisaidi ajenda kuu nne za rais Kenyatta’ amesema Atwoli .

Ameongeza kwamba Ruto haheshimu wenzake serikalini na amekuwa akiwahujumu maafisa wengine wa serikali .

“Ruto anaota mchana .anaota ..hatowahi kuwa rais wa nchi hii kubwa . Atwoli amesema

Atwoli  alikuwa ajibu madai ya Ruto kwamba hatawaogopa watu wenye ushawishi  mkubwa serikali wanaojiita ‘deep state’.