- Walimu hao wanaishi shuleni baada ya kushindwa kulipa kodi
- Obuya anaishi katika darasa moja na mkewe na watoto watatu
- Walimu wengi wa shule za kibinafsi wameathiriwa na janga la corona baada ya shule kufungwa
Walimu sita wanaishi na familia zao katika madarasa ya shule katika eneo la Uthiru ,kiambu baada ya kushindwa kulipa kodi za nyumba .
Walimu hao ni miongoni mwa wengi ambao kipato chao kilikatizwa baada ya shule kufungwa mwezi machi kwa ajili ya janga la corona .
Paul Obuya, 30, ni miongoni mwa walimu ambao wamepewa hifadhi katika shule Damacrest ambayo ni ya kibinafasi.Obuya na wenzake watano ambao hawakutaka kutajwa anasema walilazimika kuuza vitu vya nyumba ili kulipa malimbikizi ya kodi waliokuwa wakidaiwa kwa sababu hawaku na malipo ya kuendelea kugharamia kodi za nyumba zao .
Mwezi Aprili mwajiri wao Florence Wamakima aliingilia kati kwa kuwapa hifadhi kwenye baadhi ya madarasa ya shule yake na hata kuwapa chakula .
“ Hatuwezi sasa kujilipia kodi ya nyumba na mahitaji mengine ya kimsingi .mkurugenzi wetu alituruhusu kuishi katika mojawapo ya madarasa’ Obuya amesema
Amesema aliamua kuhamia shuleni humo na mkewe na watoto watatu kwa sababu hakuweza kumudu kodi ya shilingi 7000 kila mwezi .
Nimeuza karibu kila kitu cha nyumba ili kulipa deni la kodi na nikafaulu kupata shilingi elfu 10 kisha mwenye nyumba akaniruhusu niondoke’
Kabla ya janga la corona ,Obuya alikuwa akipokea mshahara wa shilingi elfu 25
Walimu hao sasa wamepewa madarasa katika ghorofa ya nne na tano katika jiengo hilo lenye madarasa , afisi ya walimu na afisi ya utawala .
Wakati mwandishi wa the star alipozuru shule hiyo walimu hao walikuwa wakiwafunza watoto mtandaoni huku familia zao zikiwa darasani .
Amesema shule huwalipa pesa kiasi za kufanya mafunzo hayo ya mtandao na anatumai mwaka ujao mambo yatakuwa sawa . Mkurugenzi Wamakima anasema wamewapa makao wafanyikazi wengine wasiokuwa walimu . Amesema kabla ya Covid 19 hakupata tatizo la kuwalipa walimu na wafanyikazi wengine lakini kwa sababu wazazi hawalipi karo baada ya shule kufungwa ,hana pesa za kuwalipa .
Wamakima anasema chaguo lake kuwapa msaada wafanyikazi wake ni kuwapa makaazi ya muda na chakula . Amesema sababu yake kuwasaidia ni kwa ajili mamake naye aliteseka sana wakati akimlea .
“ Mimi ni hasla nilizaliwa Kawangware na kuelewa na mamangu pekee .Tulikuwa watu wa kwanza kuuzwa sukuma wiki karibu na Nakumatt Prestige katika baraara ya Ngong .Mamangu hakuweza kumudu karo ya shule’ Wamakima anasema
Wamakima anasema baadaye alijiunga na Precious Blood High School ambako karo yake Ililipwa na watawa wa kanisa la katoliki .
Baadaye alikwenda chuo kikuu kwa usaidizi wa HELB na kuwa mwalimu mkuu katika shule mbali mbali za umma kati ya mwaka wa 2004 na 2014 kabla ya kuanzisha shule zake .
“ Najua umaskini ni nini baada ya kuzaliwa hohe hahe katika eneo la Gatina’ Wamakima amesema
Amesema walifunza na kuwaajiri watoto kadhaa kama njia moja ya kuirejeshea jamii .
Shule ya msingi ya Damacrest Uthiru ina walimu 177 na wanafunzi 800 .shule hiyo iliwahoji na kuwaajiri walimu 26 zaidi kwa matayarisho ya kufunguliwa kwa shule
Walimu wengi nchini hasa wa shule za kibinafasi wamejipata pabaya kwa ajili ya janga la covid 19 baada ya mishahara yao kukatizwa .
Wakamima anasimamia shule za Damacrest za msingi na upili Thogoto , Dagoretti kusini katika kaunti ya Kiambu county.