Magoha : Serikali kutoa fedha kwa shule na maski kwa wanafunzi siku ya Alhamisi

Muhtasari

 

  • Magoha asema shule za umma tayari zimepewa fedha
  • Serikali itatoa maski kwa wanafunzi kutoka familia fukara

 

Waziri wa Elimu George Magoha

 

Serikali tayari imetoa pesa za kuendesha shule za umma za msingi , amesema waziri wa elimu George Magoha . 

Waziri huyo hata hivyo hakusema ni shilingi ngapi zilizotolewa na serikali kwa shule za umma .

 
 

 “ Pesa zinafaa kuwa katika akaunti za shule leo ama kesho’ amesema Magoha akiwa Kisumu siku ya jumatano

 Fedha za  shule za upili pia zitakuwa katika akaunti za shule hizo kufikia alhamisi .Magoha ametangaza kwamba shilingi bilioni 13 zimetolewa kwa shule za sekondari .

Magoha,  alikuwa amenadamana na katibu  wa kudumu wa Mafunzo ya anuwai  Julius Jwan ili kukadiria matayariosho ya  Chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kiufundi cha kisumu

 Amesema ameridhika na matayarisho ya Chuo hicho kurejelea masomo  ya wanafunzi wake Zaidi ya 10,000

  Walimu waliripoti shuleni wiki mbili zilizopita  ili kutayarisha shule kwa uwezekano wa wanafunzi kurejea .wizara ya elimu imesema ingawaje itakuwa vigumu kuwatenganisha wanafunzi madarasani ili kuepuka mrundiko ,hilo halifai kutumiwa kama kigezo cha kuwazuia wanafunzi kurejea shuleni .

 Mtihani wa KCPE wa mwaka huu utafanywa  kuanzia machi tarehe 22 hadi tarehe 24 mwaka wa 2021  ilhali mtihani wa KCSE utaanza machi tarehe 25 hadi aprili tarehe 16 mwaka 2021 .

  Usahihishaji wa mtihani wa KCSE   utaanza aprili tarehe 19 hadi mei tarehe 7 mwaka ujao .

 
 

 Likizo ya muhula wa pili  itapunguzwa  ili kuanza disemba tarehe 23 mwaka huu na kutamatika januari tarehe 3 mwaka ujao ,amapo wanafunzi watapumzika tu kwa siku 10

 Kwa kawaida muhula hudumu kwa wiki 14 lakini sasa wanafunzi watasoma kwa wiki 11 .