'Sisi sio jamii ya kikabila,'Martha Karua apinga ripoti ya BBI

Muhtasari
  • Tunahitaji kutekeleza katiba na wala si kubadilisha katiba
  • Sisi sio jamii ya kikabila, bali viongozi wanatumia kabila hasi kama kifaa cha siasa, Martha Karua alizungumza
Martha Karua
Martha Karua

Kinara wa chama cha Narc Martha Karua amesema kuwa hatokubali marekebisho yeyote ya kikatiba yatakayo tolewa na ripoti ya BBI.

Huku kupitia ukurasa wake wa facebook kiongozi huyo alisema kwamba katiba ya mwaka wa 2010 inapaswa kutekeleza kabisa kabla ya kufikiria kurekebisha katiba hiyo.

Matamshi yake yanajiri siku moja baada ya ripoti ya BBI kuzinduliwa kirasmi katika ukumbi wa Bomas huku akiwakashifu sana viongozi kwa kueneza propaganda aliyosema ni kabila hasi.

"Ustawi unaojumuisha nchi yetu unategemea utekelezaji wa katiba na wala si kubadilisha katiba

Sisi sio jamii ya kikabila, ni viongozi ambao wanatumia kabila hasi kama kifaa cha siasa, hii ndilo tunahitaji kubadilisha kwa kuwahudumia wananchi wote sawa." Aliandika Karua.

Kiongozi huyo anaonekana kutopendezwa na mdahalo wa BBI huku akisema kuwa si mawasiliano ya nchi nzima wala ni mawasiliano ya marafiki wawili.