Msanii Christina Shusho awaomba watanzania kudumisha amani

Muhtasari
  • Christina shusho awaomba watanzania wadumishe amani wakati wa uchaguzi mkuu
  • Aliwaomba pia wagombea urais kukubali matokeo ili kusiwe na ghasia za aina yeyote
Shusho 1
Shusho 1

Mwanamuziki maarufu wa Nyimbo za Injili Christina Shusho amewaomba Watanzania wadumishe amani na wawe watulivu wanapoenda kupiga kura siku hii ya leo.

Kupitia kwenye ukurasa wake facebook Shusho aliwarai na kuwauliza wagombea urais wakubali matokeo baada ya kura ili wadumishe amani kusije tokea vurugu yeyote.

Pia aliandika  sala refu aliloandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Shusho alimshukuru Mungu kwa kuwalinda Watanzania wakati wa kampeni ambazo ziliendeshwa kwa miezi miwili.

 

"Bwana Yesu Nina kushukuru kwa kutufikisha siku ya leo, asante kwa kusikia maombi yetu na kutujibu. Miezi miwili ya campaign haikuwa rahisi, lakini kwa neema ya Mungu kazi imeisha. Najua Mungu safari uliyoanzisha utaikamilisha, mpango wako lazima uta simama. Asante Yesu kwakuwa kesho uta tupatia uchaguzi mzuri na wa amani

''Tuna kuamini wewe uliye anzisha safari salama utaimaliza salama pia. Nina waombea wagombea wote, wape utulivu na hatimaye kukubali matokeo. Asante Mungu Najua uta tenda katika jina la Yesu ninaomba."Shusho Aliandika.

Kumekuwa na wasiwasi miongoni mwa raia wa watanzania huku ikisalia saa chache ili kuamua iwapo watampa kiti rais mwingine au Pombe Mgufuli atasalia kuwa rais wao.