Moses Kuria alazimika kuahirisha mikutano yake Kahawa baada ya kuvamiwa na vijana wenye hamaki

Muhtasari
  • Moses Kuria alazimika kuahirisha mikutano yake baada ya kuvamiwa na vijana waliokuwa wamejihami na silaha
moses Kuria
moses Kuria

Drama ilishuudiwa katika eneo la Kahawa baada ya mbunge wa Gatundu Moses Kuria kulazimika kuahirisha mikutano yake baada ya kuvamiwa na vijana ambao walikuwa na silaha.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook Kuria alishtumu vikali kitendo hicho.

Kulingana na mbunge huyo alikuwa amepanga mikutano miwili ilhali nguvu zake ziliambulia patupu kwa maana maeneo hayo yalivamiwa na vijana hao.

 

"Nililazimika kughairi mkutano wangu uliopangwa na wakazi wa Kahawa wadi ya Wendani Ruiru kaunti ya KIambu

Wadi hiyo itapiga kura mnamo tarehe 15 Desemba mmoja wa wania kiti hicho Kelvin Ochieng alipanga vijana hao waje kuvamia eneo la mkutano wakiwa wamejihami na silaha

Siku chache zijazo pia nimepanga mikutano kati wadi ya Gaturi kaunti ya Murang'a ambao pia watapiga kura wiki ijayo

Nimefahamishwa kuwa uvamizi kama huo umepangwa na wafuasi wa gavana wa kaunti hiyo ishi milele BBI, ukweli tumeungana." Aliandika Kuria.

Ujumbe wake Kuria uliibua mjadala kwenye mitandao hiyo.