Enda ukatafute rika yako uachane na watoto,'Rais Uhuru awasuta wanaume wanaowanyemelea wasichana wadogo

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amekashifu vikali unyanyasaji wa watoto na kuwataka Wakenya kuungana kuwashutumu wahusika wa uovu huo katika jamii
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amekashifu vikali unyanyasaji wa watoto na kuwataka Wakenya kuungana kuwashutumu wahusika wa uovu huo katika jamii.

Akizungumza mjini Nakuru wakati wa kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani Jumatano, Rais Kenyatta aliwataja wanyanyasaji wa watoto kuwa tishio kwa ustawi wa siku za usoni wa nchi.

“Ni aibu sana kwa sisi wazee na viongozi kuskia watoto wetu wakilia kwa sababu ya tabia zetu. Ni aibu kubwa. Ni vizuri tuanze kuambiana ukweli, kwa sababu sio watoto wanajiharibu, ni sisi wazee tunaharibu watoto,

Wewe kama mzee unatembea na mtoto mdogo hata kuliko msichana wako, alafu ujiite mwanaume, wewe ni mwanaume wa saa ngapi? Si uende utafute mwenzako kama umechokeshwa na yule uko naye nyumbani? Enda utafute rika yako uwachane na watoto jameni!”

Kenyatta pia alitoa wito kwa jamii kulaani uovu huo, akisema vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia haipaswi kuachwa kwa mamlaka.

“Ukijua uko na mzee ana hizo tabia, muweke kwa soko umuanike hapo mbele ya watu wamuangalie, hiyo aibu ndiyo itafanya aache hiyo tabia,” he stated.

Hata tukisema atakaye shikwa afungwe, hiyo haitasaidia. Ile itasaidia ni sisi tubadilishe tabia zetu."