Karibuni kwenye Azimio la Umoja,gavana Kibwana awaambia viongozi wa OKA

Muhtasari
  • Hata hivyo, aliwaonya viongozi hao kuwa makini na ndege wa mapema ambao wamekuwa wakiunga mkono harakati za Azimio tangu mwanzo
Wakuu wa OKA wasaini makubaliano na kiongozi wa NARC-Kenya Martha Karua
Image: Andrew Kasuku

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana amewakaribisha viongozi wa Muungano wa One Kenya kwenye vuguvugu la Azimio La Umoja linaloongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga.

Katika taarifa yake Jumapili, gavana huyo alisema viongozi wa Oka ambao ni Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper na Gideon Moi wa KANU wanaruhusiwa kujiunga na Azimio la Umoja.

Hata hivyo, aliwaonya viongozi hao kuwa makini na ndege wa mapema ambao wamekuwa wakiunga mkono harakati za Azimio tangu mwanzo.

“Kama Mwenyekiti wa Kambi ya Kiuchumi ya Kusini Mashariki (SEKEB), na magavana wenzangu wawili Dkt Alfred Mutua, Charity Kaluki Ngilu na watu wa Ukambani, tunakaribisha OKA ndani ya AZIMIO

Maono makuu ni umoja wa kweli kuokoa na kustawisha Kenya, sio kugawana nyadhifa. Wacha washiriki wapya waheshimu Ndege za Mapema za AZIMIO," alisema.

Ripoti za viongozi wa OKA kutia saini mkataba na Azimio wa Raila zimekuwa nyingi hivi majuzi baada ya kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi pamoja na wa Ford Kenya Moses Wetang'ula kuacha vazi hilo na kujiunga na kambi ya naibu rais William Ruto.