Madaktari warejelea mgomo wao Nairobi

Kulingana na Muungano, madaktari wataitaka serikali kushughulikia masuala yanayohusu kuwapandisha vyeo madaktari ili kuhakikisha wanasonga mbele kikazi.

Muhtasari
  • Zaidi ya hayo, madaktari hao wamekanusha kuwa hazina yao ya pensheni inasalia kuwa mzozo ambao serikali inapaswa kutatua.
  • Kulingana na Muungano, madaktari wataitaka serikali kushughulikia masuala yanayohusu kuwapandisha vyeo madaktari ili kuhakikisha wanasonga mbele kikazi.
Madaktari wanaofunzwa kazini wakiongozwa na katibu mkuu wa Muungano wa Madaktari Daktari Davji Atellah na Naibu katibu mkuu Daktari Miskellah Dennis wakati wa mkutano na wanahabari jijini Nairobi Mei 9, 2023.
Madaktari wanaofunzwa kazini wakiongozwa na katibu mkuu wa Muungano wa Madaktari Daktari Davji Atellah na Naibu katibu mkuu Daktari Miskellah Dennis wakati wa mkutano na wanahabari jijini Nairobi Mei 9, 2023.
Image: STAR

Madaktari kupitia muungano wao (KMPDU) walitoa notisi ya mgomo wa siku saba siku Jumatatu.

Madaktari hao kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa KMPDU, Dennis Miskellah walisema kuwa kufuatia kukamilika kwa notisi ya siku saba, madaktari hao watapunguza huduma zao kuanzia Jumapili, Machi 9.

Kulingana na Muungano huo, madaktari wameitaka serikali kushughulikia masuala yanayohusu kuwapandisha vyeo madaktari ili kuhakikisha wanasonga mbele kikazi.

Zaidi ya hayo, madaktari hao wanaitaka serikali kuwapa bima bora ya matibabu ambayo imeripotiwa kuondolewa katika Mfuko mpya wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF).

"Tumekutana leo kama Baraza la Kamati ya Kitaifa ya Ushauri na tumekubali kufanya mgomo wetu wa nchi nzima kuanzia Jumapili wiki ijayo," alifafanua Miskellah.

Matatizo zaidi yaliyoibuliwa na watabibu hao ni pamoja na kucheleweshwa kutumwa kwa wahudumu wa afya katika hospitali za ndani ya nchi baada ya Wizara ya Afya kutaja ukosefu wa fedha za kuwezesha mchakato huo.

Miskellah pia aliongeza kuwa madaktari bado hawajatolewa kwa msaada kutoka kwa serikali katika kuhakikisha wanapata fursa za kujiendeleza kielimu kuhusiana na malipo ya ada ya uzamili na kutoa likizo ya masomo.

Zaidi ya hayo, madaktari hao wamekanusha kuwa hazina yao ya pensheni inasalia kuwa mzozo ambao serikali inapaswa kutatua.

Madaktari hao pia wanapinga shambulio la Katibu Mkuu wa KMPDU Davji Atellah na majeraha waliyopata wahudumu 25 wakati wa maandamano mnamo Februari 29.

Wakati akitoa tangazo hilo Miskellah alibainisha kuwa mgomo wa madaktari ulipangwa kufanyika baadaye mwaka huu mwezi Juni lakini kutokana na mazingira yaliyopo, ilibidi wamesongesha tarehe.