Ndugu wawili waingia mitini baada ya kumkatakata baba yao hadi kifo Kisii

Muhtasari

• Vijana wawili wanatafutwa kwa kumuuwa baba yao kwa kumkatakata kwa kisu

• Ndugu wawili hao walimvamia baba yao mwenye umri wa miaka 60 na kumnyonga hadi kufa siku ya Jumapili Januari 30 katika Kijiji cha Kiamisiori Bogetunya, katika kaunti ya Kisii.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Vijana wawili wanatafutwa kwa kumuuwa baba yao kwa kumkatakata kwa kisu.

Ndugu wawili hao walimvamia baba yao mwenye umri wa miaka 60 na kumkatakata hadi kufa siku ya Jumapili Januari 30 katika Kijiji cha Kiamisiori Bogetunya, katika kaunti ya Kisii.

Vijana hao wawili wapo mafichoni na wangali wanatafutwa na polisi.

Ndugu hao wawili Boniface Osoro na Getaro Osoro walitoweka kusikojulikana mara baada ya kisa hicho cha saa tisa alfajiri.

Kisu cha jikoni kinachoaminika kutumika na wawili hao katika utekelezaji wa unyama huo kwa baba yao mzazi kilipatikana kimeanguka sehemu ya tukio.

Kulingana na ripoti za DCI, majirani walimsikia mzee akiitisha msaada kwa kwikwi na usiahi mkali ila  baada ya kufika walimkuta mzee akiwa amelala yombo katika kidimbwi cha damu, akiwa na majeraha mabaya katika mfupa wa shingo upande wa kushoto, kifuani na kiganja cha mkono wa kulia.

Wakati huo huo, washukiwa hao ambao wamo mafichoni, wanaripotiwa kutroka kisiri kabla ya wanakijiji wenye ghadhabu kuwavamia.

Polisi wamezidisha msako mkali dhidi ya ndugu hao wawili washukiwa wa mauaji ya baba yao, huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini kiini cha mauaji hayo.