Uhuru amkosoa Ruto kuhusu miradi ya maendeleo

Muhtasari

• Kazi haifanywi juu ya magari, inafanywa ofisini," alisema Uhuru wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Wafanyakazi wa Afya huko Sarova Whitesands Mombasa.

• Kiongozi huyo wa nchi alisema Kenya imepiga hatua katika utekelezaji wa ahadi muhimu za serikali, zikiwemo huduma bora za afya kwa raia wake.

 

Uhuruto
Uhuruto

 

Rais Uhuru Kenyatta amemkashifu Naibu Rais William Ruto na viongozi wenzake wa Kenya Kwanza Alliance kwa kuendelea kukashifu utawala wake.

Kiongozi huyo wa nchi alisema Kenya imepiga hatua katika utekelezaji wa ahadi muhimu za serikali, zikiwemo huduma bora za afya kwa raia wake.

"Kazi tunafanya. Kazi haifanywi juu ya magari, inafanywa ofisini," alisema Uhuru wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Wafanyakazi wa Afya huko Sarova Whitesands Mombasa.

Rais alisema kwa sasa Kenya inapokea rufaa kutoka mataifa mengine katika eneo hilo.

"Nchini Kenya, tumeweza kuweka mifumo ya afya kwa watu wetu. Tumepiga hatua, ingawa bado hatujafikia kile tunachotaka, lakini tunaenda katika mwelekeo sahihi," Uhuru alisema.

Rais, ambaye baadaye alasiri anatarajiwa kuzindua mpango wa Huduma ya Afya kwa Wote katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Port Reitz mjini Mombasa, alisema Kenya pia ina wataalamu wa afya waliohitimu.

"Sababu kwa nini Uingereza, Kanada na Australia zinakuja kwa wauguzi wetu, ni kwa sababu wana sifa. Tunazalisha nguvu kazi yenye ubora," alisema.

 

Hata hivyo, Uhuru aliongeza kuwa kuna haja ya kuhakikisha ujuzi wa madaktari wa humu nchini unalingana na teknolojia inayotumika katika mataifa mengine.