Kulikuwa na jaribio la kuniua nikiwa na Kalonzo -Raila Odinga asema

Raila alisema maandamano yalioanza Jumatatu wiki hii sasa yatafanyika kila siku ya Jumatatu na Alhamisi.

Muhtasari
  • Alisema wakati wa maandamano ya Jumatatu, risasi zililengwa kwa magari yao lakini waliponea bila jeraha.
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga sasa anasema kulikuwa na jaribio la kumuua yeye na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Alisema wakati wa maandamano ya Jumatatu, risasi zililengwa kwa magari yao lakini waliponea bila jeraha.

"Kulikuwa na jaribio la kuua Raila Odinga na Kalonzo Musyoka. Magari yao yalipigwa risasi lakini kwa bahati nzuri hawakuguswa. Bado tunaho na kuchukizwa na hatua ya polisi," alisema.

Raila alisema haya siku ya Jumanne wakati alipokuwa akihutubia taifa.

Alilalamika kuwa wakati nchi inapitia changamoto kubwa za kiusalama kutokana na mashambulizi ya majangili Kaskazini mwa Bonde la Ufa serikali iliamua kuweka idadi kubwa ya maafisa waliotumwa kwenye maandamano ya amani.

Raila vile vile alishikilia msimamo wake wa awali kuwa maandamano yatafanyika kila siku ya Jumatatu na Alhamisi.