Fahamu nyakati Eric omondi amekamatwa na kwa nini

Kufikia sasa, mchekeshaji huyo amekamatwa takriban mara sita kuhusiana na maandamano.

Muhtasari

•Jumatatu, mchekeshaji  Eric Omondi , alitiwa mbaroni kwa mara nyingine baada ya kuandamana jijini Nairobi.

•Siku ya Jumanne wiki iliyopita, alikamatwa kwa mara ya tatu akielekea Ikulu.

Nyakati Eric Omondi amekamatwa na kwa nini
Image: WILLIAM WANYOIKE

Siku ya Jumatatu, mchekeshaji aliyegeuka kuwa mwanaharakati, Eric Omondi , alitiwa mbaroni kwa mara nyingine baada ya kuandamana jijini Nairobi.

Eric alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Central baada ya kukamatwa na maafisa wa polisi siku ya Jumatatu asubuhi. Alikuwa akiandamana dhidi ya gharama ya juu ya maisha wakati ambapo alikamatwa.

Hii ilikuwa ni mara ya nne kwa mchekeshaji huyo mkongwe kukamatwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Hapo awali alikamatwa mara tatu kuhusiana na maandamano ya kupinga gharama ya juu ya maisha.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita, alikamatwa kwa mara ya tatu akielekea Ikulu. Alikuwa akivuta mkokoteni wa mbao aliodai kuwa umebeba CV takriban milioni tatu za vijana wanaotafuta kazi. Nia yake kuu ilikuwa ni kuziwasilisha Ikulu.

Kufikia sasa, mchekeshaji huyo amekamatwa takriban mara sita kuhusiana na maandamano.