Wanasiasa maarufu ambao walihudhuria harusi ya Akothee

Jumla ya watu wasiopungua 300 walikuwa wamealikwa.

Muhtasari

•Akothee na Dennis Shweizer walifunga pingu za maisha kwenye harusi ya kifahari iliyofanyika Windsor Golf Hotel & Country Club, Nairobi.

•Zaidi ya wanasiasa 10 maarufu walihudhuria harusi ya pili ya Akothee.

Wanasiasa maarufu waliohudhuria harusi ya Akothee
Image: WILLIAM WANYOIKE

Siku ya Jumatatu, mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee na mchumba wake Dennis Shweizer almaarufu Omosh walifunga pingu za maisha kwenye harusi ya kifahari iliyofanyika Windsor Golf Hotel & Country Club, Nairobi.

Harusi ya pili ya mwimbaji huyo ambayo ilifanyika mnamo siku yake ya kuzaliwa ya 43 ilipambwa na wanafamilia, marafiki wa karibu, wasanii maarufu na wanasiasa mashuhuri nchini. Jumla ya watu wasiopungua 300 walikuwa wamealikwa.

Zaidi ya wanasiasa 10 maarufu walihudhuria harusi ya pili ya Akothee.