Wanajeshi wa Uganda wahukumiwa kifungo kwa kuwaua waandamanaji

Muhtasari

• Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewatia hatiani wanajeshi wawili kwa mauaji ya watu watatu wakati wa maandamano mwaka jana.

• Mwanajeshi wa kwanza alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumuua Grace Waiona katika duka la kutengeneza magari - akidaiwa kuwa muandamanaji.

 

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewatia hatiani wanajeshi wawili kwa mauaji ya watu watatu wakati wa maandamano mwaka jana.

Maandamano hayo yalianza kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais wa wakati huo Robert Kyagulanyi, ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine, katika mkutano wa kampeni.

Mwanajeshi wa kwanza alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumuua Grace Waiona katika duka la kutengeneza magari - akidaiwa kuwa muandamanaji.

Pia alimpiga risasi Hussein Ssenoga - mfanyakazi mwenzake ambaye alikataa kusaidia katika kukamatwa.

Askari wa pili alikuwa mwanachama wa Kitengo cha Ulinzi cha Mitaa. Alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kumuua Ibrahim Kirevu - mwanaume ambaye alitakiwa kumsindikiza kwenye kituo cha polisi.

Hizi ni hukumu za kwanza kuhusiana na mauaji yaliyotekelezwa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya mwaka jana.