Ukraine: Marekani yaagiza familia za wafanyakazi wa ubalozi kuondoka Ukraine, huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka

Muhtasari

• Kuna ripoti kuwa Urusi inapanga kuchukua hatua muhimu ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

• Jumamosi, tani zipatazo 90 za ''misaada hatari'' ya Marekani zikiwemo risasi kwa ajili ''walinzi wa mstari wa mbele'' ziliwasili Ukraine.

• Russia imekanusha madai kwamba inapanga kuivamia Ukraine.

Wahudumu wasio wa lazima wa ubalozi wa Marekani mjini Kyiv wamepewa ruhusa ya kuondoka chini ya hatua mpya.
Wahudumu wasio wa lazima wa ubalozi wa Marekani mjini Kyiv wamepewa ruhusa ya kuondoka chini ya hatua mpya.
Image: GETTY IMAGES

Marekani imewaagiza ndugu wa wafanyakazi wa ubalozi wake nchini Ukraine kuondoka nchini humo huku hali ya wasi wasi ikiendelea kungezeka katika kanda hiyo.

Wizara ya mambo ya nje pia imetoa ruhusa kwa wahudumu wasio wa lazima kuondoka na kuwataka raia wa Marekani waliopo nchini Ukraine kuangalia uwezekano wa kuondoka.

Katika taarifa yake, imesema kuwa kuna ripoti kuwa Urusi inapanga kuchukua hatua muhimu ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Russia imekanusha madai kwamba inapanga kuivamia Ukraine.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imewaonya watu wasisafiri kwenda Ukraine na Urusi kutokana na hali ya wasi wasi inayoendelea na ''uwezekano wa unyanyasaji dhid ya raia wa Marekani ".

"Kuna taarifa kuwa Urusi inapanga kuchukua hatua muhimu ya kijeshi dhidi ya Ukraine," lilisema taarifa ya ushauri ya Wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliliambia Shirika la habari la AFP kwamba ubalozi unaendelea kuwa wazi lakini akaridia tahadhari kutoka ikulu ya White House kwamba uvamizi unaweza kuja " katika wakati wowote ule'".

Walisema kuwa serikali "haitakuwa katika nafasi ya kuwaokoa raia wa Marekani katika hali kama hiyo ya dharura ".

Jumamosi, tani zipatazo 90 za ''misaada hatari'' ya Marekani zikiwemo risasi ziliwasili Ukraine
Jumamosi, tani zipatazo 90 za ''misaada hatari'' ya Marekani zikiwemo risasi ziliwasili Ukraine

Mkuu wa muungano wa ulinzi wa kijeshi wa NATO, ameonya kwamba kuna hatari ya mzozo mpya Ulaya baada ya vikosi vya Urusi vinavyokadiriwa kuwa 100,000 kukusanyika mpakani.

Jumamosi, tani zipatazo 90 za ''misaada hatari'' ya Marekani zikiwemo risasi kwa ajili ''walinzi wa mstari wa mbele'' ziliwasili Ukraine.

Waziri wa Mambo yanje wa Marekani Anthony Blinken alisema serikali inakusanya "msururu wa hatua ambazo zitabaini mahesabu ya Putin" ikiwa ni pamoja na kuongeza ulinzi katika Ukraine kwa usaidizi zaidi wa kijeshi.

Urusi iliwahi kuchukua eneo la Ukraine kabla , ambalo liliitenga na Ukraine katika mwaka 2014, baada ya nchi hiyo kumpindua rais aliyeungwa mkono na Urusi.

Tangu wakati huo, jeshi la Ukraine limekuwa katika vita na waasi wanaoungwa mkono na Urusi katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo karibu na mipaka yake na Urusi.

Inakadiriwa kuwa watu 14,000 waliuawa katika jimbo ka Donbas kufuatia mzozo huo.

Rais wa Marekani Joe Biden amekwishasema kuwa yatakuwa maafa kwa Urusi iwapo itafanya uvamizi zaidi katika Ukraine
Rais wa Marekani Joe Biden amekwishasema kuwa yatakuwa maafa kwa Urusi iwapo itafanya uvamizi zaidi katika Ukraine

Jumapili, Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza ilimshutumu Bw Putin kwa kupanga kumteua kiongozi anayeungwa mkono na Urusi kuiongoza serikali ya Ukraine.

Mawaziri wa Uingereza wameonya kwamba serikali ya Urusi itakabiliwa na adhari iwapo uvamizi utafanyika.