Watu 26 wafariki DRC baada ya kuangukiwa na waya ya umeme sokoni

Muhtasari
  • Watu 26 wafariki DRC baada ya kuangukiwa na waya wa umeme sokoni
  • Haijawa wazi ni nini kilichosababisha kukatika kwa waya wa umeme
Image: BBC

Takriban watu 26 wamefariki baada ya kupigwa na umeme baada ya kukatika na kuanguka kwa waya wa umeme katika soko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, polisi imesema.

Waya uliokuwa na kiwango cha juu cha umeme ulikatika ghafla na kuangukia ndani ya nyumba na watu waliokuwa wakinunua bidhaa karibu na mji mkuu Kinshasa Jumatano.

Picha ambazo hazijathibitishwa zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha hali baada ya tukio hilo, huku miili kadhaa ikionekana kwenye vidim bwi vya maji.

Haijawa wazi ni nini kilichosababisha kukatika kwa waya wa umeme.

Lakini taarifa, iliyotolewa na kampuni ya taifa ya umeme ya DRC imesema kuwa inaamini radi ilipiga sehemu ya waya huo, na kusababisha uanguke ardhini. Kampuni hiyo imetma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa wa mkasa huo.

Polisi ilisema kuanguka huko kwa waya kulitokea katika wilaya ya Matadi-Kibala iliyopo viungani mwa mji mkuu Kinshasa na kwamba watu kadhaa walifariki mara moja.