Uchaguzi wa Nigeria 2023:Obi kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani

Peter Obi wa chama cha Labour aliibuka wa tatu katika kura zilizopigwa Jumamosi.

Muhtasari

• Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walisema kumekuwa na mapungufu makubwa katika mchakato wa uchaguzi.

Peter Obi mgombea wa urais wa chama cha Labour.
Peter Obi mgombea wa urais wa chama cha Labour.
Image: AFP

Chama cha upinzani cha Labour nchini Nigeria kinatarajia kupinga ushindi wa Bola Tinubu wa chama tawala cha APC katika uchaguzi wa rais. Peter Obi wa chama cha Labour aliibuka wa tatu katika kura zilizopigwa Jumamosi. Upinzani unasema matokeo yalichakachuliwa;na wanataka warudie kupiga kura upya. Ni 28% tu ya wapiga kura walioshiriki kupiga kura Nigeria.

Wengine hawakuweza kupiga kura kwa sababu ya ubovu wa mashine.

Bw Tinubu alipata mgao wa kura 37%, ikiwa ni idadi ndogo ya ushindi kuliko marais waliopita wa Nigeria.

Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walisema kumekuwa na mapungufu makubwa katika mchakato wa uchaguzi, na kuongeza kuwa kumekuwa na ununuzi wa kura lakini ilikuwa mapema mno kusema jinsi hali hiyo ilivyoenea.

Chama cha wafanyakazi cha Nigeria kinachoongozwa na mgombea urais Peter Obi kitawasilisha pingamizi la kisheria dhidi ya kuchaguliwa kwa rais mteule, Bola Tinubu, mgombea makamu wa rais wa chama hicho alisema Jumatano.