Fahamu jinsi Laura Mattarella,Bintiye rais wa Italia,alivyokuwa Mama taifa wa Italia

Mamake alifariki mwaka wa 2012 kabla babake kuwa rais

Muhtasari

•Laura Mattarella wako nchini Kenya kwa ziara ya siku nne,aliandamana na babake, Sergio Mattarella.

Laura Materella ni binti wa Rais wa Italia, Sergio Matarella na pia anahudumu kama Mama taifa wa jamuhuri ya Italia.

Je ni kwa nini anaitwa Mama taifa na ilhali ni binti wa Rais?

Rais  Mattarella ni mjane. Mkewe, Marisa Chiazzese, alifariki mwaka 2012, miaka mitatu kabla ya kuwa rais.

Laura Mattarella amekuwa karibu na baba yake ambaye amekuwa rais tangu mwaka wa 2015.

Aliposhika wadhifa huo, rais alimteua Laura kuchukuwa majukumu rasmi ya mama wa taifa.

Laura Mattarella ni wakili kitaaluma na ameolewa kwa Cosimo Comello na wana watoto watatu.

 Amekuwa akiandamana na baba yake katika safari za Kiserikali. Kuna wakati pia amehudhuria mikutano bila baba yake katika nafasi yake kama Msaidizi wa Rais wa Italia.

  Italia sio nchi pekee kuwa na Mama taifa mbaye sio mke wa rais. Katika historia ya Marekani, imetokea mara tisa. Aliyejulikana zaidi alikuwa Harriet Lane, mpwa wa James Buchanan; ambaye alikaimu kama Mke wa Rais katika kipindi chake kama Rais kati ya 1857 na 1861.

Buchanan alikuwa rais pekee wa Marekani aliyehitimu maisha yake yote. Lane, ambaye pia anaitwa "Malkia wa Kidemokrasia" katika rekodi za historia, inasemekana alihuisha utawala wa Buchanan kwa kupamba upya Ikulu ya White House na kuandaa karamu maarufu za chakula cha jioni. 

Laura Mattarella pamoja na baba yake,Sergio Mattarella ,wako nchiniKenya kwa ziara ya siku nne.Waliokolewa katika ikulu ya Nairobi na Rais William Ruto pamoja na Mama taifa Rachel Ruto.Kwa heshima ya Rais huyo,Rais Ruto aliandaa karamu katika Ikulu ya Nairobi kwa ajili ya Sergio.