Polisi wa Uganda wafanya majaribio ya kutuliza maandamano ya kupinga gharama ya maisha

Polisi walisema wanajiweka tayari kukabiliana na waandamanaji iwapo maandamano hayo yatatokea nchini humo.

Muhtasari

• Uganda sasa wanalenga kujiunga na Kenya, Afrika Kusini, Senegal, Nigeria na Tunisia katika maandamano ya mirengo ya upinzani.

wakishika doria jijini Nairobi mnamo Machi 27, 2023.
Polisi wakishika doria jijini Nairobi mnamo Machi 27, 2023.
Image: EZEKIEL AMINGA

Taarifa kutoka nchini Uganda zinaarifu kwamab polisi nchini humo wamefanya majaribio jinsi ya kutuliza maandamano yanayotarajiwa kufanyika katika miji mikuu ya taifa hilo kupinga gharama ya juu ya maisha.

Maandamano hayo yameuwa yakitajwa kwamba huenda yatafanyika hivi karibuni, sambamba nay ale ambayo yameitishwa nchini Kenya na mrengo wa upinzani ukiongozwa na Raila Odinga.

Kurugenzi za polisi, kama vile Kitengo cha Jeshi la Polisi na Kurugenzi ya Kupambana na Ugaidi, zilifanya mazoezi ya pamoja katika kituo cha mafunzo huko Kigo, Wilaya ya Wakiso, jana ambapo vitengo vyote viwili vilionyesha uwezo wao wa kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi na maandamano kwa wakati mmoja. Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Meja Jenerali Geoffrey Katsigazi, alishuhudia binafsi mazoezi hayo, jarida la Monitor lilisema.

Polisi wanahisi kwamba kumekuwa na mikutano ya kisiri baina ya makundi ya upinzani ambayo inalenga kuanzishwa kwa maandamano ya kupinga gharama ya juu ya maisha.

Iwapo Uganda itafanikisha kufanya maandamano hayo, basi itakuwa imejiunga kwenye orodha ya mataifa mengi ambayo wiki jana yalizindua kampeni zao za maandamano dhidi ya utawala uliopo madarakani.

Mataifa kama vile Afrika Kusini, Nigeria, Senegal na Tunisia yalijiunga na Kenya katika maandamano dhidi ya setikali zilizopo madarakani, maandamano hayo yakiongozwa na viongozi wa upinzani katika mataifa husika, huku lalama kuu ikiwa ni gharama ya juu ya maisha miongoni mwa masuala mengine tata.