Zamana kutoka Tanzania ashinda tuzo ya kifahari ya kifalme mjini London

Zamana, Kijana mmoja kutoka Tanzania ameshinda Tuzo ya Uwezeshaji kwa Wanawake ya Amal Clooney

Muhtasari

• Tuzo za kila mwaka za Prince's Trust hutambua vijana ambao wamefaulu licha ya hali ngumu , kuboresha nafasi zao maishani na kuwa na matokeo chanya kwa jamii zao.

• Kufuatia hafla hiyo, Zamana baadaye Jumatano atakutana na Mfalme Charles III wakati wa mapokezi katika Jumba la Buckingham kusherehekea mafanikio ya washindi.

Zamana, msicha kutoka Tanzania aliyeshinda tuzo za Amal Clooney
Zamana, msicha kutoka Tanzania aliyeshinda tuzo za Amal Clooney
Image: BBC

Zamana, Kijana mmoja kutoka Tanzania ameshinda Tuzo ya Uwezeshaji kwa Wanawake ya Amal Clooney huko London kwa juhudi zake za kusaidia elimu ya wasichana.

Tuzo za kila mwaka za Prince's Trust hutambua vijana ambao wamefaulu licha ya hali ngumu , kuboresha nafasi zao maishani na kuwa na matokeo chanya kwa jamii zao

Zamana alitambuliwa baada ya kuzindua kampeni yake ya kusaidia na kuhimiza wasichana kusalia shuleni nchini Tanzania.

Kupitia kampeni yake ya “Niruhusu Nisome”, Zamana analenga kuwasaidia wasichana wa shule na wazazi wao kuelewa umuhimu wa kukamilisha masomo yao.

“Tuzo hii ina maana kubwa sana kwangu.Kila msichana katika jamii yangu ana ndoto ya maisha yake ya baadaye, kama vile wasichana ulimwenguni kote.Ndoto yangu ni wasichana wengi kusalia shuleni,” Zamana alisema baada ya kupokea tuzo hiyo Jumanne usiku katika ukumbi wa michezo wa London Royal Drury Lane.

Kufuatia hafla hiyo, Zamana baadaye Jumatano atakutana na Mfalme Charles III wakati wa mapokezi katika Jumba la Buckingham kusherehekea mafanikio ya washindi.

Ilianzishwa na Mfalme, Prince's Trust International inasaidia vijana katika nchi 18 kupitia programu za ajira, elimu na biashara.