Joe Biden aamrisha Uganda kufutilia mbali sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Biden aliwasihi watu wote kote ulimwenguni kumuunga mkono ili kushinikiza viongozi wa taifa hilo kufutilia mbali sharia hiyo.

Muhtasari

• Biden alilishtumu taifa hilo kwa kupitisha sheria hio ambayo inawapa adhabu kali kwa mtu yoyote atakaye husika na vitendo vya mapenzi baina ya watu wa jinsia moja.

• Sheria hiyo iliyopitishwa Jumatatu pia ililenga kwenda mbali zaidi na kuwafanya watu kuwa wahalifu kwa msingi ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais Yoweri Museveni.
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais Yoweri Museveni.
Image: MAKTABA

Siku moja tu baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini sheria kali inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja nchini humo, Rais wa Marekani Joe Biden ameamrisha sheria hio ifutiliwe mbali.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Biden alilishtumu taifa hilo kwa kupitisha sheria hiyo ambayo inampa adhabu kali mtu yoyote atakaye husika na vitendo vya mapenzi baina ya watu wa jinsia moja.

‘’Kupitishwa kwa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu, watu wa Uganda hawastahili hili. Pia inahatarisha matarajio ya ukuaji wa uchumi wa nchi nzima,’’ ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Biden pia aliwasihi watu kote duniani kumuunga mkono ili kushinikiza viongozi wa taifa hilo kufutilia mbali sheria hio mpya.

‘’Ninaungana na watu ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na wengi nchini Uganda, kotoa wito wa kutupiliwa mbali mara moja kwa sheria hiyo,’’

 Biden aliongeza kuwa tangu kupitishwa kwa sheria hiyo watu wengi wanadhaniwa kuhusika na mapenzi ya jinsia moja tayari wameanza kubaguliwa na kughulumiwa.

Biden pia aliongeza kuwa kupitishwa kwa sheria hii itaendeleza ukiukwaji wa haki za kibinadamu ambayo kulingana naye itaongeza kesi dhidi ya haki za kibinadamu na ufisadi nchini Uganda.

‘’Sheria hii ya aibu ni maendeleo ya aibu ya hivi punde katika mwenendo wa kuogopesha wa ukuikwaji wa haki za binadamu na ufisadi nchini Uganda,’’Biden aliongeza.

Watu watakaopatikana kuhusika katika mapenzi ya jinsia moja kuhudumu kifungu cha maisha gerezani.

Sheria hiyo iliyopitishwa Jumatatu pia ililenga kwenda mbali zaidi na kuwafanya watu kuwa wahalifu kwa msingi wa utambulisho wao wa kijinsia.

 baadhi ya sheria zilizotiwa saini jumatatu na Rais Yoweri ni;

  • Mtu anayepatikana na hatia ya kulea au kusafirisha watoto kwa madhumuni ya kuwashirikisha katika vitendo vya wapenzi wa jinsia moja anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
  • Watu binafsi au taasisi zinazounga mkono au kufadhili shughuli au mashirika ya haki za LGBT, au kuchapisha, kutangaza na kusambaza nyenzo na fasihi za vyombo vya habari vinavyounga mkono wapenzi wa jinsia moja, pia watakabiliwa na mashtaka na kufungwa gerezani.