Serikali yateketeza shamba la miraa ekari 535 katika msako wa kupambana dawa za kulevya

Maafisa wa kupambana na dawa za kulevya walivamia shamba hilo kwa panga na mashine za misumeno, wakakata na kisha kuteketeza miraa mazima.

Muhtasari

• Hio limevutia maoni kinzani kutoka kwa baadhi ya watu hadharani ambao wanahisi kwamba mirungi haina madhara mengi ikilinganishwa na bangi.

Tanzania yateketeza shamba la miraa.
Tanzania yateketeza shamba la miraa.
Image: STAR

Serikali ya taifa jirani la Tanzania limeteketeza shamba lenye ukubwa wa ekari 535 amablo lilikuwa limepandwa miraa au mirungi katika msako wa kupambana na dawa za kulevya nchini humo.

Operesheni hiyo ya kukomesha matumizi ya mirungi kama dawa za kulevya imekuwa ikifanyika kwa Zaidi ya wiki moja katika mkoa wa Kilimbanjari, kaskazini mwa taifa lenye kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika video ambazo zimesambazwa mitandaoni na ambazo zinaonesha zoezi hilo likiendeshwa na maafisa kutoka idara ya kupambana na dawa za kulevya nchini humo, maafisa waliokuwa wamevalia magwanda rasmi ya kijani walionekana wakilivamia shamba hilo kwa panga na misumeno, kukata miti ya mirungi kabla ya kulitia moto.

Taifa la Tanzania kwa muda limeshikilia msimamo wake kwamba mirungi ni moja ya dawa za kulevya ambazo zimekatazwa katika taifa hilo kwa kile wanahisi ina madhara mengi hasi.

Hio limevutia maoni kinzani kutoka kwa baadhi ya watu hadharani ambao wanahisi kwamba mirungi haina madhara mengi ikilinganishwa na bangi.

Wengine waliikosoa serikali kwa kuchukua hatua hiyo ya kuharibu mirungi badala ya kuikuza na kuiuza kwa mataifa jirani ya Kenya na Somalia ambayo yana watumizi wengi.

Nchini Kenya, Mirungi au miraa kwa jina linguine ni moja ya kilimo ambacho kinafanywa kwa wingi katika kaunti za Meru na Tharaka Nithi, Embu, Kirinyaga na sehemu za Isiolo na inauzwa kama bidhaa kwa watumizi humu nchini na hata nje ya nchi katika soko kubwa la Somalia.