Wanafunzi 90 mahututi baada ya kulishwa keki yenye bangi

Wanafunzi hao walidaiwa kununua keki hizo kutoka kwa mchuuzi wa kando ya barabara karibu na shule hiyo na baadae wakaanza kupiga chafya na kupata kichefuchefu.

Muhtasari

• Mahakama ya juu zaidi ya Afrika Kusini mwaka 2018 ilihalalisha matumizi ya bangi na watu wazima katika maeneo ya faragha.

• Pia ilihalalisha upandaji wa bangi kwa matumizi ya kibinafsi.

Mamlaka ya polisi nchini Afrika Kusini imeanzisha uchunguzi katika tukio la kuhuzunisha ambalo limesababisha wanafunzi takribani 100 kulazwa hospitlini kutokana na chakula.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchino humo, watoto 90 wa shule moja kaskazini mwa mji mkuu wa Pretoria walipelekwa hospitalini baada ya kula keki zinazodhaniwa kukwekwa chembechembe za dawa ya kulevya aina ya bangi.

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Pulamadibogo walikimbizwa katika hospitali za mitaa siku ya Jumatano baada ya kupata kichefuchefu na kuumwa na tumbo na kutapika, idara ya elimu ya mkoa wa Gauteng ilinukuliwa na vyombo vya habari.

Walifikiri kuwa walinunua keki hizo kutoka kwa mchuuzi wa barabarani walipokuwa wakienda shuleni.

"Kwa hakika, hili linatuhusu na tunaomba uvumilivu wakati uchunguzi unaendelea na wanafunzi wanaendelea kupata nafuu," alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Elimu ya Gauteng (MEC) Matome Chiloane.

"Tunawasihi wanafunzi kuwa waangalifu na kile wanachonunua na kutumia."

Polisi waliitwa shuleni wakati wa kisa hicho na mshukiwa alitambuliwa.

Mahakama ya juu zaidi ya Afrika Kusini mwaka 2018 ilihalalisha matumizi ya bangi na watu wazima katika maeneo ya faragha. Pia ilihalalisha upandaji wa bangi kwa matumizi ya kibinafsi.