Hafla ya harusi yageuka mazishi Bw. Harusi akimpiga risasi Bi. Harusi, mamake na dadake

Mwnaamume huyo ambaye ni mwanariadha mlemavu baadae alijiua kwa bunduki pia na inaarifiwa Bi harusi alikuwa amemmshinda kwa miaka 15.

Muhtasari

• Chaturong alikuwa mdogo kwa miaka 15 kuliko bi harusi, gazeti la Bangkok Post liliripoti.

• Chaturong na Kanchana walikuwa wameishi pamoja kwa miaka mitatu kabla ya kufunga ndoa, BBC iliripoti, ikitoa mfano wa vyombo vya habari vya Thailand.

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Mwanariadha mlemavu aliyetuzwa wa Thailand alimuua bibi harusi wake na watu wengine wanne kwenye tafrija ya harusi yao kabla ya kujigeuzia bunduki, polisi walisema Jumatatu kwa mujibu wa BBCNews

Chaturong Suksuk, 29, mshindi wa medali ya fedha ya ASEAN Para Games, alimpiga risasi bibi harusi Kanchana Pachunthuek kwenye harusi kaskazini mashariki mwa Thailand siku ya Jumamosi, mamlaka ilisema.

Wahasiriwa wengine walitambuliwa kama mama wa bi harusi Kingthong Klajoho, 62, dadake mdogo Kornnipa Manato, 38, na mgeni, Thong Nonkhunthod, 50, Bangkok Post iliripoti.

"Walikuwa na mabishano kuhusu masuala ya kibinafsi na Chaturong alitembea hadi kwenye gari lake na kuchukua bunduki kabla ya kufyatua risasi," alisema Matichon Wongbaokul, afisa wa polisi kutoka mkoa wa kaskazini mashariki wa Nakhon Ratchasima.

Alisema Chaturong alimpiga risasi bibi harusi wake na wengine wanne kabla ya kujiua.

Mmoja wa wahasiriwa alikuwa mgeni aliyepigwa na risasi iliyopotea.

Polisi waliambia BBC kwamba Chaturong "alikuwa amelewa sana wakati huo," lakini nia yake hasa haijafahamika. Alikuwa amenunua bunduki na risasi kihalali mwaka jana, polisi walisema.

Chaturong alikuwa mdogo kwa miaka 15 kuliko bi harusi, gazeti la Bangkok Post liliripoti.

Chaturong na Kanchana walikuwa wameishi pamoja kwa miaka mitatu kabla ya kufunga ndoa, BBC iliripoti, ikitoa mfano wa vyombo vya habari vya Thailand.

Akiwa muogeleaji, alishinda medali mbili za fedha katika Michezo ya ASEAN Para ya 2022 huko Indonesia na Kambodia.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa alikuwa mgambo wa jeshi la Thailand, na alikuwa amepoteza mguu wake wa kulia alipokuwa akishika doria kwenye mipaka.

Ufyatuaji wa risasi ni nadra sana nchini Thailand, lakini umiliki wa bunduki ni jambo la kawaida nchini humo, kulingana na BBC.

 

Mwezi uliopita, watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi katika jumba la kifahari huko Bangkok, BBC iliripoti. Na mnamo Oktoba 2022, polisi wa zamani aliwaua watoto 37 katika shambulio la bunduki na visu kwenye kitalu kaskazini mashariki mwa Thailand.