Safari za ndege zasitishwa na kutatizika baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel

EasyJet imesitisha safari za ndege kwenda na kutoka Tel Aviv hadi na ikijumuisha Jumapili, 21 Aprili.

Muhtasari
  • Wizz Air ilisema itaanza tena safari za kuelekea Israel Jumanne, 16 Aprili baada ya kusimamisha safari za ndege kuelekea Tel Aviv siku ya Jumapili na Jumatatu.

Abiria wa mashirika ya ndege wanakabiliwa na kuahirishwa au kutatizwa kwa safari za ndege kuelekea Israel na nchi jirani baada ya mashambulizi ya anga ya Iran mwishoni mwa juma.

EasyJet imesitisha safari za ndege kwenda na kutoka Tel Aviv hadi na ikijumuisha Jumapili, 21 Aprili.

Wizz Air ilisema itaanza tena safari za kuelekea Israel Jumanne, 16 Aprili baada ya kusimamisha safari za ndege kuelekea Tel Aviv siku ya Jumapili na Jumatatu.

Hata hivyo, ilionya: "Abiria wanaweza kupata mabadiliko fulani ya ratiba."

Wizz Air ilisema kuwa "inafuatilia kwa karibu hali hiyo na mamlaka husika na kuwafahamisha abiria wake kuhusu mabadiliko yote ya ratiba".

"Abiria wote walioathiriwa na mabadiliko ya ratiba watapewa chaguzi za kuweka tena nafasi au kurejeshewa pesa," iliongeza.

Israel ilifunga anga yake Jumamosi jioni baada ya Iran kufanya shambulio la kwanza kabisa la moja kwa moja dhidi ya nchi hiyo. Iran ilirusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel kulipiza kisasi shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Tehran mjini Damascus tarehe 1 Aprili, ambalo liliua baadhi ya makamanda wakuu wa Iran.

Israel haijasema ilitekeleza shambulio hilo la ubalozi mdogo, lakini inaaminika kuwa ndiyo iliyohusika .