Zaidi ya watu 2,000 taabani baada ya kukumbwa na maporomoko ya udongo Burundi

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano alifariki Ijumaa usiku, na zaidi ya watu 2,400 sasa hawana makazi.

Muhtasari

•Kulingana na mkuu wa manispaa hiyo Muhuta Niyonsavye Scholastique, sasa watu wa familia 350 hawajulikani walipo kufuatia tukio hilo.

Image: BBC

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano alifariki Ijumaa usiku, na zaidi ya watu 2,400 sasa hawana makazi.

Hii ni baada ya Udongo kuporomoka kutoka kwenye mlima mdogo Gabaniro uliopo kwenye eneo na kisha udongo wake kuanguka n katika eneo la Gitaza katika manispaa ya Muhuta katika jimbo la Rumonge magharibi mwa Burundi.

Kulingana na mkuu wa manispaa hiyo Muhuta Niyonsavye Scholastique, sasa watu wa familia 350 hawajulikani walipo kufuatia tukio hilo.

"Mlima wote wa Gabaniro wumeporomoka " na mashamba ya zaidi ya heka 500 yamesombwa, aliiambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha Udongo ukisukumwa na wakazi wanaolia wakiomba msaada.

Mkuu wa manispaa ya Muhuta anasema hivi sasa wakazi 2,485 wamepata hifadhi katika shule ya Ecofo Kirasa wakiwa bila mahitaji yoyote, wakisubiri msaada.