Wamalawi watoa heshima za mwisho kwa makamu wa rais aliyefariki katika ajali ya ndege

Saulos Chilima, 51, alichukuliwa kuwa pumzi ya hewa safi katika siasa za Malawi.

Muhtasari

•Ibada katika Uwanja wa Taifa wa Bingu ilianza kwa salamu za heshima kutoka kwa familia yake.

Image: BBC

Maelfu ya Wamalawi wanashiriki katika ibada ya mazishi katika uwanja wa kitaifa kutoa heshima kwa makamu wa rais aliyefariki katika ajali ya ndege wiki iliyopita.

Saulos Chilima, 51, alichukuliwa kuwa pumzi ya hewa safi katika siasa za Malawi.

Alikuwa mzungumzaji fasaha na mwanakampeni mwenye nguvu ambaye alikuwa na nguvu kubwa miongoni mwa vijana ambao ni zaidi ya nusu ya Wamalawi.

Alikuwa Mkatoliki mcha Mungu..Atazikwa katika wilaya yake ya Ntcheu, kilomita 180 kusini mwa Lilongwe siku ya Jumatatu, ambayo imetangazwa kuwa mapumziko ya umma.

Ibada katika Uwanja wa Taifa wa Bingu ilianza kwa salamu za heshima kutoka kwa familia yake.

Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 41,000 umejaa, huku watu wengi wakiwa nje.

Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera nyekundu, kijani kibichi na nyeusi ya Malawi, lililetwa ndani ya uwanja na kikosi cha jeshi la heshima.

Image: BBC

Mwanawe, Sean, alikumbuka jinsi alivyokuwa baba mwenye upendo, jinsi alivyokuwa na wakati wa watoto na kucheza nao michezo.

Aliongeza kuwa baba yake amekuwa na ushindani mkubwa na alitaka kushinda kila wakati. "Baba alikuwa mchapakazi ambaye kila mara alihakikisha kwamba anafanya jambo," alisema.

Kaka yake, Ben, alisema familia inashukuru kwa kupewa vitu vyake binafsi alivyokuwa navyo wakati wa ajali, ikiwamo saa yake ya mkononi na rozari.