Utata huku mtoto wa mwezi 1 akifariki baada ya mamake kumweka kwenye jiko "kimakosa"

Mariah alisema alikuwa akimlaza mwanawe chini ili alale na kwa bahati mbaya akamuweka kwenye oveni badala ya kitanda.

Muhtasari

•Ripoti kutoka Marekani zinasema kuwa mwanamke huyo, aliyetambulika kama Mariah Thomas, alimweka mtoto wake mchanga katika tanuri mapema wiki iliyopita.

•Inaripotiwa kwamba Mariah alikuwa akimlaza mtoto wake na kwa bahati mbaya akamuweka kwenye tanuri badala ya kitanda cha kulala.

Mshukiwa Mariah Thomas
Image: JACKSON COUNTY DETENTION CENTRE

Mwanamke mwenye umri wa miaka 26 kutoka jiji la Kansa, jimbo la Missouri, nchini Marekani ameshtakiwa kwa kosa la jinai baada ya kudaiwa kumlaza mtoto wake wa mwezi mmoja kwenye oveni badala ya kitanda na kusababisha kifo chake.

Ripoti kutoka Marekani zinasema kuwa mwanamke huyo, aliyetambulika kama Mariah Thomas, alimweka mtoto wake mchanga katika tanuri mapema wiki iliyopita..

Mwendesha Mashtaka wa Kaunti ya Jackson Jean Peters Baker alitangaza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Jumamosi kuwa polisi walimpata mtoto huyo siku ya Ijumaa baada ya kupokea simu ya 911 iliyoripoti mtoto mchanga asiyepumua. Walipowasili, maafisa wanasemekana kugundua mtoto huyo akiwa na majeraha ya moto.

Maafisa waliambiwa kwamba Thomas alikuwa akimlaza mtoto wake chini kwa ajili ya kulala na kwa bahati mbaya akamuweka kwenye tanuri badala ya kitanda cha kulala.

Idara ya Zimamoto ya Jiji la Kansas, ambayo pia ilifika katika eneo la tukio hilo, ilitangaza kwamba mtoto huyo alikufa katika eneo la tukio.

“Mwathiriwa alipatikana sebuleni akiwa amelala kwenye kiti cha gari, karibu na mlango wa mbele. Alikuwa amepata majeraha ya joto kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake,” ripoti ya polisi ilisomeka.

Ilisomeka zaidi, "Alikuwa amevaa vazi la mwili juu ya nepi. Nguo hiyo ilionekana kuyeyuka kwenye nepi, na ilikuwa chafu sana, kuna uwezekano ilichomwa upande wa nyuma. Blanketi la mtoto likiwa na alama kubwa za kuungua."

Kabla ya polisi kufika, walisema katika taarifa yao kwamba babu wa mtoto huyo alirudi nyumbani na alikuwa akisikia harufu ya moshi nyumbani. Baadaye alimkuta mtoto amekufa kwenye kitanda chake.

Inaripotiwa kwamba Thomas alisema kwamba alimweka kwenye oveni kwa bahati mbaya.

Kulingana na mwendesha mashtaka, Thomas sasa anakabiliwa na kosa la hatari A la kuhatarisha maisha ya Mtoto katika kiwango cha kwanza 1. Iwapo atapatikana na hatia, mshukiwa atapokea kifungo cha chini cha miaka 10 na kifungo cha juu zaidi cha maisha.