Jamaa wa miaka 35 akamatwa kwa kumbaka mwanamke wa miaka 50 hadi kufa

Kulingana na ripoti ya polisi, James anadaiwa kumbaka mwenzake Deborah hadi kufa kabla ya kuutupa mwili wake kwenye shimo la taka.

Muhtasari

• Polisi waliongeza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 17, 2024.

• Alifikishwa mahakamani mnamo Alhamisi, Januari 31 kujibu mashtaka ya ubakaji na mauaji.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mwanamume mwenye umri wa miaka 35 nchini Nigeria katika jimbo la Ondo ameripotiwa kutiwa nguvuni na polisi kwa tuhuma za kumbaka rafiki yake wa kike mwenye umri wa miaka 55 hadi kufa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ndani, James Emmanuel alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkuu wa Jimbo la Ondo kujibu mashtaka yanayohusiana na kifo cha mfanyakazi mwenzake, Bi Deborah Abiodun.

Kulingana na ripoti ya polisi, James anadaiwa kumbaka mwenzake Deborah hadi kufa kabla ya kuutupa mwili wake kwenye shimo la taka.

Polisi waliongeza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 17, 2024.

Alifikishwa mahakamani mnamo Alhamisi, Januari 31 kujibu mashtaka ya ubakaji na mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Anwana Josephine, aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 17, 2024 majira ya saa tano usiku, kosa kinyume na Kifungu cha 357 na adhabu yake chini ya Kifungu cha 358 cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura. 37, Juz. 1 Sheria za Jimbo la Ondo la Nigeria, 2006, chanzo hicho kiliripoti.

"Kwamba wewe, James Emmanuel, katika tarehe, muda na mahali pale katika Wilaya ya Hakimu iliyotajwa hapo juu ulimuua Deborah Abiodun kwa kumpiga na jiwe kichwani na kutupa maiti yake ndani ya shimo la taka na hivyo kufanya kosa kinyume na sheria. Kifungu cha 316 na adhabu yake chini ya Kifungu cha 319 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura. 37, Juz. 1 Laws of Ondo State of Nigeria, 2006,” ilisoma sehemu ya hati ya mashtaka.

Hata hivyo, wakati akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkuu F.A. Aduroja aliwaruhusu polisi kuendelea kumzuilia mshukiwa katika kituo cha kurekebisha tabia kilichopo Ondo mjini.

Kesi hiyo iliahirishwa huku mshukiwa akisubiri kusikilizwa Machi 27, 2024.