Pasta Kanyari akukutana ana kwa ana ndani ya korti na mshukiwa wa mauaji ya dadake (video)

Hata hivyo, Matara ambaye alionekana akiwa nadhifu kwa suto nyeusi na nywele zilizochanwa vizuri alikanusha mashtaka dhidi yake .

Muhtasari

• Mahakama iliweka tarehe mpya, Februari 26 kama siku ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ili kubaini hatima ya John Matara. 

John Matara akutana uso kwa uso na pasta Kanyari, kakake Starlet Wahu.
MAHAKAMANI// John Matara akutana uso kwa uso na pasta Kanyari, kakake Starlet Wahu.
Image: Screengrab//CITIZENTVKENYA

Mchungaji Victor Kanyari kwa mara ya kwanza walikutana na mshukiwa mkuu katika mauaji ya dadake, Starlet Wahu, John Matara.

Kukutana kwao kwa hali ya ukakasi mwingi kulijiri katika mahakama ya Milimani Ijumaa ambapo Matara alikuwa anasomewa mashtaka ya mauaji ya mwanasosholaiti Wahu baada ya uchunguzi kukamilika.

Hata hivyo, Matara ambaye alionekana akiwa nadhifu kwa suto nyeusi na nywele zilizochanwa vizuri alikanusha mashtaka dhidi yake akijitetea kwamba yeye siye aliyesababisha kifo cha kikatili cha dadake pasta Kanyari.

Upande wa mashtaka wa serikali ulitaka mshukiwa azuiwe kupata uhuru kwa masharti ya dhamana. Wakati wote wa kesi hiyo, Matara aliyevalia nadhifu alionekana akiwa ameketi kwa wasiwasi huku shtaka likisomwa.

Katika video hiyo, kwa upande mwingine alionekana Pasta Kanyari ambaye alikuwa anafuatilia kwa umakini mkubwa kesi hiyo ikisomwa na waliangaliana na Matara ana kwa ana.

Mahakama iliweka tarehe mpya, Februari 26 kama siku ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ili kubaini hatima ya John Matara.

Tazama video hii hapa jinsi Matara walikutana ana kwa ana na pasta Kanyari, kakake na marehemu Wahu;