Naibu Gavana wa Kisii Robert Monda apinga kuondolewa ofisi mahakamami

Muhtasari

• "Ndiyo tulifanya maombi na hakimu akakubali Machi 26, 2024, kama tarehe ya kusikilizwa," alisema Wilkins Achoki mmoja wa mawakili wawili wanaomtetea Dkt Monda.

Robert Monda akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi yake katika bunge la Seneti mnamo Machi13 2024/ Picha: EZEKIEL AMING'A
Robert Monda akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi yake katika bunge la Seneti mnamo Machi13 2024/ Picha: EZEKIEL AMING'A

Mawakili wanaomwakilisha Monda walisema kwamba walikuwa wametuma maombi ya kusikilizwa kwa kesi ya mteja wao mbele ya Jaji Teresa Odera katika Mahakama ya Kisii Jumanne jioni.

"Ndiyo tulifanya maombi na hakimu akakubali Machi 26, 2024, kama tarehe ya kusikilizwa," alisema Wilkins Achoki mmoja wa mawakili wawili wanaomtetea Dkt Monda.

Monda pia anawakilishwa na Katwa Kigeni.

"Ndiyo tulifanya maombi na hakimu akakubali Machi 26, 2024, kama tarehe ya kusikilizwa," alisema Wilkins Achoki mmoja wa mawakili wawili wanaomtetea Dkt Monda.

Monda anafanya juhudi zake za mwisho kuokoa maisha yake ya kisiasa baada ya Seneti kuunga mkono kuondolewa kwake baada ya mijadala ya siku mbili.

Naibu Gavana huyo alifurushwa na Seneti kutokana na nguvu ya ushahidi uliotolewa kuhusu madai kwamba alipokea hongo ya Sh800,000 kutoka kwa Dennis Mokaya kwa ahadi ya kumpatia wadhifa wa meneja wa kibiashara katika Kampuni ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Gusii.

Pia alishtakiwa kwa kuchochea kukamatwa na kuzuiliwa kwa kaka yake, Reuben Monda, kwa kukata baadhi ya miti kwenye ardhi ya familia miongoni mwa mashtaka mengine.

Gavana wa Kaunti ya Kisii Simba Arati anatarajiwa kuchapisha kwenye gazeti la Serikali kuwa nafasi ya naibu gavana iko wazi na kuanzisha harakati za kutafuta naibu gavana mwingine kufikia Alhamisi wiki hii.

Likitokea pengo katika afisi ya naibu gavana, katiba inawapa magavana uhuru wa kufanya uteuzi mpya ndani ya siku 14 kuchukua nafasi ya naibu gavana.

Naibu huyo anaweza kuwa amejiuzulu, amefariki akiwa madarakani au ameshtakiwa.

Wateule hao watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Kaunti ndani ya siku 60.