Mshutuko wa moyo

Butwaa: Nilivyojipata katika ndoa ya jamaa aliyekuwa na mke na watoto wanne

Makubwa ya jiji huyajui hadi uyabebe mwenyewe

Muhtasari

 

  • Kufupisha kisa ,siku hiyo Nasieku aligundua kwamba ‘mume’ wake alikuwa pia na mke wa kwanza na watoto wanne!
  • Edward alijua kushawishi na baada ya  muda wa miezi mitatu ,msichana alianza kujiona kama mke mtarawajiwa wa Edward .
  • Msichana alibeba vyote vyake na kupewa mshahara wake wa mwisho na mwajiri wake na hata kununuliwa zawadi kadhaa za kuanza maisha ya ‘ndoa’ kama ‘Mke wa mtu’.

 

Kuna msemo kwamba miji ina mambo ,usipojua basi utajilaumu . Ndio hali ambayo  Nasieku anaikumbuka akijicheka hadi sasa kwani haamini kwamba yaliomsibu yamefanyika na hawezi kubadilisha lolote .

 Alikuja mjini Nairobi kufanya kazi kama yaya katika mtaa wa Highridge na baada ya miaka mitatu akifanya kazi hiyo aliamua basi alikuwa ameshafanya kwa muda wa kutosha na tayari kuanza maisha ya ndoa kama mke wa mtu . Ni katika Pilka pilka hizo za kutongozwa na wanaume wa kila aina alipoamua kwamba yeye sasa angekubali posa ya  Edward ,jamaa mmoja aliyekuwa akisimamia mafundi wa mjengo katika mtaa huo .

 Ziara nyingi za kila jumapili kwenda kati kati ya jiji la kununuliwa vitamu kama kuku na  vibanzi ndo uliokuwa mtindo wake wa wikendi. Edward alijua kushawishi na baada ya  muda wa miezi mitatu ,msichana alianza kujiona kama mke mtarawajiwa wa Edward . Kila kitu kilikuwa shawrai hata akaanza kuwa mgeni wa kila mara katika nyumba ya Edward katika maa wa Zimmerman . Angeamua kuitumia siku yake ya kupumzika jumapili kwenda kwa Edward na kumfulia na kufanya usafi ni kana kwamba amelipwa .

 Uziri  na ukarimu wa Edward ulimfanya mtoto wa kik kujiamulia kwamba hatangoja kuulizwa swali kama wanavyofanya wazungu kwamba ‘Will you marry me?’ ,Alianza mwenyewe kubebeba virago vyake pole pole ,nguo baada ya nyingine hadi kwa Edward . Alijua sasa huyu ndio mume  na hakuona pingamizi .Edward naye aliendelea kumpa presha akimtaka aache kazi kabisa na waazne kuishi kama mke na mume .

  Nasieku hakujua kwamba jiji lina wenyewe ,  baada ya kuamua kumuarifu mwajiri wake kuhusu uamuzi wake wa kwenda kuoelewa  na kuacha kazi ,alijua kwamba mkondo wake wa kuanza maisha ya ndoa ulikuwa shwari . Msichana alibeba vyote vyake na kupewa mshahara wake wa mwisho na mwajiri wake na hata kununuliwa zawadi kadhaa za kuanza maisha ya ‘ndoa’ kama ‘Mke wa mtu’.

 Siku moja  baada ya miezi miwili ya kuishi pale kama mke wa Edward , Nasieku alimuona  mwanamke mmoja akisaidia kuingiza begin a nguo na sanduku   katika ploti alimokuwa akiishi . Kando yake ,watoto wanne wanaofanana na wote walikimbia wakielekea katika mlango wa chumba chao na Edward .walishangaa kumhusu kwa sababu alikuwa amesimama mlangoni ni kama kuwazuia wasiingie lakini hakujua kinachofanyika . Mwanamke yule alipomaliza kumlipa boda boda ndipo alipogeuka na kuja moja kwa moja kuingia katika nyumba ambayo Edward na Nasieku walikuwa wakiita yao .  Kufupisha kisa ,siku hiyo Nasieku aligundua kwamba ‘mume’ wake alikuwa pia na mke wa kwanza na watoto wanne! Mke wa kwanza alikuwa amekuja jijini tena kwa sababu ilikuwa ni disemba wakati wa likizo sasa watoto wamekuja kumuona baba yao . Yaliishia kwa machozi na kwa sababu ya kushangaa na ule mshutuko wa kupata zile habari kwa njia ile ,Nasieku alirejea kutuliza fikra kwa majiri wake .