Chupi Mkobani

Unajitetea vipi? Jinsi mpango wa kando alivyonitega kwa kuweka chupi yake kwenye mkoba wangu

Julius hakujua kwamba chupi ile ilikuwa mtego kwake

Muhtasari

 

  •  Nusra ajipate mashakani kwa kitendo kile cha mpango wa kando 
  •  Julius kwa sasa anazingatia kumaliza uhusiano wake na mwanamke huyo wa pembeni 
  • Mkewe sasa anafuatilia kwa makini kila anachofanya 

 

 Julius amejipata katika mtego  ambao hajui atajitoa vipi lakini umempa  funzo kuhusu atakavyoshughulikia masuala yake siku zijazo .

 Amekuwa katika uhusiano haramu wa pembeni na mwanamke mwingine al maarufu mpango wa kando .Kwa muda mrefu sasa mke huyo wa pembenei amekuwa akimpa presha kwamaba wanafaa kufanya uhusiano wao kuwa rasmi na wa wazi ili naye pia atambuliwe kama mke wake . Julius hata hivyo amekuwa akikwepa suala hilo jambo ambalo limemhahamakisha mpenzi huyo wake wa pembeni kwa sababu tayari ana mke na hataki kujenga uhasama na mkewe kwa kujitokeza wazi kwamba anataka kuoa mke wa  pili

 Katikla njia moja ya kuonyesha kwamba hajafurahia kujikokota kwa Julius kuchukua hatua ya haraka kumfanya kuwa mke rasmi ,mpango huyo wa kando maajuzi amefanya jambo ambalo limeitia hatarini ndoa ya Julius . Baada ya kwenda kwake kumtembelea na kuwa huko wikendi nzima ,mwanamke huyo wa pembeni alichukua chupi yake ya ndani na kuiweka katika mkoba wa Julius . Alipofika nyumbani mkewe ambaye hutumia mkoba huo kumpakia chakula ,alikutaa na chupi ya mwanamke .

 Ugomvi ulianzia hapo kwani Julius hakujua atakavyojitetea lakini alifahamu fika kwamba aliyemfanyia  unyama huo ni mpango wake wa kando . Hasira zake hazikumsaidia wakati huo kwa sababu lengo la mwanamke huyo wa kando lilikuwa kwamba mkewe Julius aipate ile chupi ile pazuke ugomvi na hata labda Julius na mkewe watengane ili yeye sasa apate fursa ya kuitwa mke wa Julius .

 Julius anasema alifaulu kumshawishi mkewe kwamba kwamba mkoba ule uliazimwa na rafiki yake kazini na huenda ndiye anayefahamu jinsi chupi ileilivyojipata mle ndani .Kwa shingo upande mke wake alikubali kijisababu hicho lakini Julius anafahamu sasa kwamba kuanzia pale ,kila hatua anayopiga itakuwa ikichunguzwa kwa makini na mkewe . Mke wake sasa ameanza kukagua kwa uangalifu nguo zake wakati anapozifua na hata kuzinusa  ilia pate usahidi kwamba anafanya chezo chezo lolote njje ya doa yao .

 Iwapo kuna  kuponea ambako kumempa afueni basi ni huko kwani chupi hiyo nusra ingevunja ndoa yake lakini sasa ana  mawazo kuhusu jinsi ya kukata uhusiano na mwanamke yule wa pembeni