- Mama mkwe ndiye aliyeamua shule ambako mtoo wao wa kwanza alipelekwa na hata gharama ya shule .
- Anapokuja kuwatembelea ,mama mkwe huamua kila chakula wanachoandaa na Elziabeth anahisi sasa kwamba mama ya mume wake anamsakama na kuivuruga ndoa yake .
Ndoa ukiwa nje huonekana kuwa kitu kizuri sana na hakuna mabaye huweza kutabiri au kujua baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kuleta msukosuko katika uhusiano kati ya mume na mke .
Wakati watu wanapofanya mipango ya kufunga pingu za maisha ,wengi hujua kwamba basi wamefika mwisho kuhusu kuwahi kumtafuta mtu mwingine wa kuwahi kuishi naye maisha yao yote .wengia wakati huo wa mwanzo mwanzo huwa hawafikirii kwamba wakati mwingine kuna sababu au watu wengine ambao huweza kuwa na ushawishi mkubwa wa kutengeza ama kuvunja ndoa yao .
Kwa Elizabeth Kawira* amejifunza hilo akiwa ndani ya ndoa baada ya kubainika wazi kwamba uhusiao wake na mama mkwe wake hautawahi kuboreka kwa sababu mama mkwe ndiye amekuwa akiendesha kila hatua katika maisha yao .
Elizabeth anasema walipoona na Francis, hapakuwa na ishara kwamba mamake atakuwa na usemi kupindukia katika maisha yao na kila jambo lilionekana kuwa la kawaida ila muda ulipozidi wakiwa katika ndoa ,amegundua kwamba maamuzi yote kuhusu maisha yao lazima yaidhinishwe na mama mkwe kwani Francis hawezi katu kufanya lolote kabla ya kushauriana na mamake kwanza .
Elizabeth anasema mtindo huo wa ndoa yao umekuwa ukivuruga uhusiao kati yake na mume wake kwa sababu wakati mwingine yaonekana ni kana kwamba ndoa yao ni mume moja na wake wawili . Mama mkwe ndiye aliyeamua shule ambako mtoo wao wa kwanza alipelekwa na hata gharama ya shule . Anapokuja kuwatembelea ,mama mkwe huamua kila chakula wanachoandaa na Elziabeth anahisi sasa kwamba mama ya mume wake anamsakama na kuivuruga ndoa yake .
Anaogopa kumzungumza na mume wake kuhusu tabia za mamake kwani anasema juhudi zake za kumuelea kuhusu baadhi ya vitendo vyake vya kumhusisha mamake katika masuala yao havipendezi zimefeli na alichukulia kwa ubaya kwani aliona ni kana kwamba mke wake alikuwa analenga kumtenganisha na mamake .
Mama mke amekuwa akitoa matamshi ya kushangaza wakati mwingine na msimamo wake kuhusu mambo hayo haujakuwa ukimpeneza Elizabeth . kwa mfano ,mpango wa Elizabeth na mume wake kufungua akaunti ya pamoja ya benki ili kuaza kuweka akiba ya waoa siku za baadaye ulitibuka wakati Francis alipomueleza mamake kuhusu hilo . Mamama mke alifoka sana akidai Elizabeth alikuwa na njama za kuiba pesa za mwanawe na hivyo ndivyo mipango yao mingi ilivyofeli .
Anasema anampenda mume wake na hana nia ya kuondoka lakini kutokana na jinsi mama mkwe alivyowasakama kwa kuingilia kila uamuzi na hatua wanazofanya ,huenda akalazimika kuchukua hatua kal na hivi karibuni atalazimika kumtaka mumewe achague kati yake na mamake .