Mbona watu hutumiana picha za utupu?

Mpenzi wangu alikuwa akiwanasa wanaume kwa picha zake za utupu

Muhtasari
  •  Hata hivyo  kiliingia mchanga kitumbua wakati alipogundua vitabia vidogo vodogo ambavypo mwanzoni havikumtisha hasa lakini vilimpa wasi wasi kidogo .
  •  Oyoo amefika kiwango cha kusema huenda hatowahi kuoa kwa sababu ya  alichofanyiwa na  mwanamke ambaye alikuwa amempenda  kwa dhati .

 

Joe Oyoo* Alipata  mshutuko ambao hadi sasa bado unamutua hata usingizini baada ya  kujipata katika hali ya  kutisha . baada ya kuwa katika uhusiano  na  mpenzi wake kwa mia miwili ,daalili zilikuwa nzuri kwamba walikuwa katika mkondo ufaao kuboresha uhusiano wao hata Zaidi na walikuwa wameanza kuzungumza kuhusu maisha ya baadaye pamoja .

 Hata hivyo  kiliingia mchanga kitumbua wakati alipogundua vitabia vidogo vodogo ambavypo mwanzoni havikumtisha hasa lakini vilimpa wasi wasi kidogo . Mpenzi wake alianza kuwa muangalifu na simu yake ya mkononi na wakati mwingi aliizima  akienda bafuni au hata kuificha . Mwanzoni mwa uhusiano wao hakuna aliyekuwa ameweka  nywila katika simu yake ya mkononi na yeyote kati yao angeichukua simu ya mwenzake na kuichakura bila kuwepo hofu ya lolote .

Tabia hiyo ya kuanza kuficha ficha simu na kuizima ilimfanya Oyoo ashuku kwamba palikuwa na jambo baya lililokuwa likifanyika na alichofanya baadaye kilimuacha na majuto na kuathiri uwezo wake kabisa kuwahi tena kumuamini mwanamke yeyote .

 

 Oyoo kupitia rafiki yake anayejua mambo ya  teknolojia aliweza kuunganisha mawasiliano ya whatsapp ya simu ya mpenzi wake na  tarakilishi bebe yake iliyokuwa nyumbani ili kumwezesha kupata jumbe zote za whatsapp za mpenzi wake  na kujua yote kuhusu mawasiliano yake ya simu . Wiki moja baada ya oparesheni hiyo ya kuiduakua simu ya mpenzi wake kufanywa Oyoo alianza kazi yake ya ujasusi na muda sio mrefu alichokipata kilimuacha kinywa wazi lakini pia kilimvunja moyo na tangu hapo hajawahi kabisa kuaini tena mapenzi .

 Mpenzi wake alikuwa akizituma picha zake akiwa uchi kwa wanaume wengine! Jambo ambalo lilimkera sana ni kwamba  hakuwa tu anazituma picha hizo kwa mtu mmoja bali kwa Zaidi ya wanaume wawili .

‘ Kwa sababu ya heshima iliyokuwepo katika uhusiano wetu ,sikuwahi hata kuitisha picha zake  akiwa uchi,lakini nilishangaa kuona kwamba alipiga picha akiwa uchi wa mnyama kuwatumia wanaume wengine …nilikereka sana’ anasema Oyoo .

 Akiwa na ushahidi huo alifikiri kwamba mpenzi wake labda angejutia anachofanya na  baada ya Oyoo kumhoji kuhusu alichokuwa akifanya ,mpenzi wake alikana kabisa kuwasiliana au kufanya lolote baya na watu wengine . Alianza hata kububujikwa machozi akishangaa mbona Oyoo alikuwa akimshuku na kumshtumu kwa  mambo ambayo hakufahamu chimbuko lake . Oyoo hakuamini jinsi mpenzi wake alivyokuwa hana haya kabisa ya kukana kwamba hakuwa akifanya lolote baya licha ya ushahidi ambao alikuwa nao na alipomuonyesha ,mambo yalibadilika

 Mpenzi wake huyo alianza kuomba msamaha  akisema hatowahi kurudia tena kufanya hayo lakini ilikuwa wazi kwamba ule ndio uliokuwa mwisho wa uhusiano wao na ilikuwa kama muda wote huo  ulikuwa umetupwa kwa ajili ya vitendo vya mtu mmoja katika uhusiano wao .

 Ndoto za Oyoo kuwahi kuoa na kumuamini mwanamme zilikatikia hapo na hadi wakati huu kumbukumbu zozote kuhusu kujipata katika uhusiano zinamtia machungu  kwani anasema miaka mitatu baada ya tukio hilo yungali ana makovu sana na woga wa kumuamini mwanamke .

 Oyoo amefika kiwango cha kusema huenda hatowahi kuoa kwa sababu ya  alichofanyiwa na  mwanamke ambaye alikuwa amempenda  kwa dhati .