Kwanini watu waliochanjwa bado wanapata Corona

Muhtasari

• Kutokana na rekodi za kila siku za visa vipya vya Covid-19 katika nchi kama vile Ufaransa na Uingereza, ufanisi wa chanjo kwa mara nyingne tena umekuwa mada ya kujadiliwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii.

Chanjo bado zinaufanisi kwa kiasi kikubwa katika kuzuwia kuugua sana kutokana na Covid-19
Chanjo bado zinaufanisi kwa kiasi kikubwa katika kuzuwia kuugua sana kutokana na Covid-19
Image: GETTY IMAGES

Dunia inapitia wimbi jipya la janga la Covid-19. Nchi kama vile Marekani , Ufaransa, Uingereza, Brazil na nchi nyingine nyingi zimeshuhudia ongezeko la visa vya maambukizi kutokana na aina mpya za cvirusi vya corona za delta na omicron.

Hata hivyo wanasayansi, madaktari, na taasisi za huduma za afya wanaendelea kutegemea aina mbali mbali za chanjo ambazo tayari zimefanyiwa majaribio na kuidhinishwa kote duniani kuwalinda watu dhidni ya maambukizi.

Ufuatao ni uchambuzi wa jinsi walivyojiandaa kusaidia kudhibiti janga

Utata usio sahihi unaongezeka

Kutokana na rekodi za kila siku za visa vipya vya Covid-19 katika nchi kama vile Ufaransa na Uingereza, ufanisi wa chanjo kwa mara nyingne tena umekuwa mada ya kujadiliwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii.

Huku baadhi ya watumiaji wakikosoa hatua zilizowekwa na mamlaka za kudhibiti maambukizi, baadhi wanapinga uwezekano wa madhara ya chanjo.

Chanjo zinaendelea kuwakinga watu dhidi ya madhara ya Covid
Chanjo zinaendelea kuwakinga watu dhidi ya madhara ya Covid
Image: GETTY IMAGES

Hadi sasa, athari kuu zilizoshuhudiwa ni ndogo na hutoweka baada ya siku chache. Miongoni mwa malalamiko makuu ya athari za chanjo ni : maumivu, uvimbe katika eneo ilipochomwa sindano ya chanjo, homa, maumivu ya kichwa, mchoko, maumivu ya mwili, kuhusi baridi mwilini na kichefuchefu.

Matukio mabaya zaidi kama vile kuganda kwa damu mwilini na myocarditis (majeraha ya moyo) ni jambo linalochukuliwa kama la nadra na maafisa wa afya na faida za kupata dozi za chanjo ni kubwa zaidi kuliko hatari, wanasema.

BBC ilizungumza na daktari bingwa wa watoto na magonjwa ya maambukizi Renato Kfouri kuhusu ufanisi wa chanjo zilizopo sasa na ukweli watu waliochanjwa wanapata na kusambaza virusi vya corona.

Alisema kwamba wimbi la kwanza la chanjo dhidi Covid -19, ambalo lilijumuisha chanjo za Pfizer, AstraZeneca, na Janssen miongoni mwa nyingine, zililenga kupunguza hatari ya mtu kuugua sana ugonjwa wenyewe, ambao una uwezekano kumfanya mtu alazwe hospitalini na hata kufariki.

"Chanjo hulinda vyema mtu dhidi ya kuugua sana na badala yake huumwa kwa kiwango cha kawaida, kidogo au hata kumfanya asipate aina za dalili zozote za Covid. ," anasema Kfouri, ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Brazili la chanjo.

Lengi kuu la hizi chanjo , kwahivyo halikuwa kuzuwia maambukizi yenyewe, bali kuyafanya maambukizi ya virusi vya corna kuwa yasiyo ya madhara makubwa kwa mwili.

Lengo hili ni sawa na lengo la chanjo ya mafua, ambayo imekuwepo kwa miongo kadhaa.

Dozi, ambayo hutolewa kila mwaka, sio lazima izuwie maambukizi ya virusi vya mafua ya Influenza, lakini huzuwia madhara yake kwa makundi ya watu wanaoweza kuathiriwa zaidi, kama vile watoto , wanawake wajawazito na wazee.

Kwa kuangalia kwa mapana zaidi, ulinzi huu dhidi ya kuugua sana una athari za moja kwa moja kwa mfumo mzima wa afya: kupunguza maambukizi mabaya ya mfumo wa upumuaji kunakwenda sambamba na idadi ndogo ya wagonjwa katika vyummba vya wagonjwa mahututi, uhitaji mkubwa wa upatikanaji wa vitanda vya wagonjwa wa dharura katika wodi za kuwahudumia na kutoa muda zaidi kwa ajili ya wahudumu wa afya wa kuwatibu wagonjwa ipasavyo.

Na data zinaonyesha kwamba chanjo zinasaidia vyema: kulingana na mfuko wa Jumuiya ya madola, dozi dhdi ya virusi vya corona zilizuwia , kufikia Novemba 2021, jumla ya vifo milioni 1.1 na watu milioni 10.3 kulazwa hospitalini nchini Marekani pekee.

Kituo cha Ulaya cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (ECDC) na Shirika la afya duniani (WHO) wanakadiria kuwa watu 470,000 wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wamenusurika katika nchi 33 kote barani Ulaya tangu chanjo dhidi ya Covid ilipoanza kutolewa.

Nini kinaelezea hali ya sasa?

Ni dhahiri kwamba maambukizi ya kujirudia ya mara kwa mara au kupatikana na maambukizi miongoni mwa watu kumeongezeka katika nyakati za hivi karibuni, na hili linaweza kuelezewa kwa njia tatu.

Njia ya kwanza ni rahisi: watu kwa kawaida walikusanyika na kusherehekea katika kipindic ha Mwaka mpya na Krismasi. Hili lenyewe, liliongeza hatari ya kusambaa kwa virusi vya corona.

Jambo la pili, takriban mwaka mmoja baada ya kupatikana kwa chanjo katika baadhi ya maeneo ya dunia, wataalamu waligundua kwamba kinga ya mwili dhidi ya Covid baada ya kuchanjwa haidumu daima. "Baada ya muda, tumeshuhudiakwamba kiwango cha kinga kinapungua.

Kupungua huku kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa au cha chini kulingana aina ya chanjo na umri wa mtu binafsi ," anaelezea Kfouri.

"Hii inaonyesha haja ya kupata dozi ya tatu, kwanza kwa wazee na wenye kinga ya mwili ya kiwango cha chini, na baadaye kwa watu wote wazima," aliongeza daktari.

Kigezo cha tatu kinahusiana na kuwasili kwa aina mpya ya omicron, ambayo inasambaa zaidi na ambayo inaonekana chanjo za awali za Covid hazina ufanisi kwake wa kutosha.

"Kutokana na suala la kwamba watu waliochanjwa hupata maambukizi linapaswa kuangaliwa kama kitu cha kawaida na tutahitajika kujifunza kuishi na hali hii ," anasema Kfouri.

"kwa bahati nzuri, ongezeko la hivi karibuni katika maambukizi ya Covid limesababisha kiwango kidogo cha watu wanaolazwa hospitalini na vifo, hususan miongoni mwa watu ambao tayari wamekwishapata chanjo ," anasema.

"Chanjo inaendelea kuwalinda watu dhidi ya kuugua sana , kama ilivyotarajiwa," alihitimisha. Chati kutoka mfumo wa huduma ya afya ya New York inaonyesha wazi ufanisi wa chanjo, ikionyesha utofauti wa viwango vya maambukizi ya Covid, kulazwa kwa wagonjwa na vifo vya watu waliopata chanjo na ambao hawakupata chanjo.

Mwanzoni mwa mwezi wa Disemba ,idadi ya wagonjwa waliolazwa na vifo katika jiji la New York vilipanda kwa kiwango kikubwa miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo.