Orodha ya watumishi wa umma waliojiuzulu ili kugombea viti vya kisiasa

Muhtasari

•Hatimaye muda ambao tume ya uchaguzi nchini (IEBC)  ilikuwa imepatia watumishi wa umma wanaokusudia kuwania kujiuzulu ulifika kikomo siku ya Jumatano.

Waziri Sicily Kariuki,John Munyes na George Natembeya wamejiuzulu
Waziri Sicily Kariuki,John Munyes na George Natembeya wamejiuzulu
Image: THE STAR

Hatimaye muda ambao tume ya uchaguzi nchini (IEBC)  ilikuwa imepatia watumishi wa umma wanaokusudia kuwania kujiuzulu ulifika kikomo siku ya Jumatano.

Katika kipindi cha mwezi mmoja ambacho kimepita watumishi wengi wa umma ikiwemo mawaziri wameacha nafasi walizokuwa wameshikilia ili kuangazia kampeni zao.

Hii hapa orodha ya watumishi wa umma ambao walichukua hatua hiyo kufikia siku ya mwisho ya Februari 9, 2022.

•Charles Keter – Waziri wa ugatuzi

• John Munyes- Waziri wa petroli na uchimbaji madini

• Cicily Kariuki - Waziri wa maji na usafi wa mazingira

•Adan Mohammed - Waziri wa ukuzaji wa viwanda

• Joseph Boinet – Katibu mwandamizi wizara ya utalii

• Wavinya Ndeti - Katibu mwandamizi wa uchukuzi

• Joseph Boinnet - Katibu mwandamizi wa Utalii

Aliyekuwa polisi IG Joseph Boinnet ambaye anatafuta tiketi ya UDA kuwa gavana wa Elgeyo Marakwet.
Aliyekuwa polisi IG Joseph Boinnet ambaye anatafuta tiketi ya UDA kuwa gavana wa Elgeyo Marakwet.
Image: Mathews Ndanyi

• Gideon Mung'aro- Katibu mwandamizi wa ugatuzi

• Hassan Noor Hassan- Katibu mwandamizi wa elimu

•Ken Obura - Katibu mwandamizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

• Patrick Ntuntu-  Katibu mwandamizi wa kazi

• John Musonik - Katibu mwandamizi wa petroli na uchimbaji madini

• George Natembeya - Kamishna wa eneo la bonde la ufa

• Hussein Dado - Katibu Mwandamizi wa masuala ya ndani

• Hamadi Boga - Katibu wa kudumu wa ukulima