Athari za kiafya zinazoambatana na kutumia sukari haramu

Shirika hilo lilibadilisha msimamo na kusema sukari hio inapaswa kubadilishwa kuwa ethanol ya viwandani.

Muhtasari

• Sukari hio iliyokamatwa na shirika hilo mwaka wa 2018 ilistahili kuharibiwa ama kurudishwa katika nchi ilyotoka kulingana na sheria.

• Shirika hilo lilibadilisha msimamo na kusema sukari hio inapaswa kubadilishwa kuwa ethanol ya viwandani.

Baadhi ya sukari iliyoharibika ambayo ilinaswa na maafisa wa DCI.
Baadhi ya sukari iliyoharibika ambayo ilinaswa na maafisa wa DCI.
Image: DCI

Jumatano, Rais William Ruto aliwapiga kalamu wahudumu wa serikali 27 baada ya kushukiwa kuhusika katika Sakata ya kuachilia sukari iiyokuwa imekamatwa na Shirika la Viwango la Kenya (KEBS).

Sukari hio iliyokamatwa na shirika hilo mwaka wa 2018 ilistahili kuharibiwa ama kurudishwa katika nchi iliyotoka kulingana na sheria.

Hata hivyo, shirika hilo lilibadilisha msimamo na kusema sukari hiyo ingebadlishwa kutumika kwa utengezaji wa kemikali aian ya ethanol. 

Licha ya mifuko hiyo ya sukari kuwekewa alama 'si salama kwa matumizi ya binadamu' wauzaji reja reja wanadaiwa kupakia upya sukari kwenye pakiti za kilo 1 na 2 za chapa ya sukari za humu chini miongoni mwao Kabras, Mumias Sugar na West Sugar na kuwauzia wakenya.

Lakini je, wafahamu athari za kutumia sukari hii?

Baadhi ya athari hizi ni:

Kama sukari hiyo ina chembechembe za zebaki (Mercury), sumu yake inaweza kuishia kuharibu mfumo wa fahamu wa mtu, kuwasababishia kupooza na kuhatarisha watoto ambao bado hawajazaliwa. Inaweza pia kusababisha Hyperactivity Disorder (Ugonjwa wa Upungufu wa Makini) kwa Watoto.

Pia kama sukari hio ina chembechembe za shaba inaweza kusababisha uharibifu wa ini, maumivu ya tumbo, kuhisi kichefuchefu, kuhara na kutapika.

Sukari hiyo ikiweza kuwa na Ukungu (Moulds) unaweza kuathirika na matatizo ya kupumua.

Sukari hio pia inashukiwa kuwa na chachu (yeast) hii inaweza kuathiri viungo vya ndani vya mwili.