Benki ya Ethiopia yawaaibisha wateja waliochukua pesa wakati wa hitilafu ya kiufundi

Notisi zenye majina na picha zao zilionekana nje ya matawi ya Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE) siku ya Ijumaa.

Muhtasari

•Benki ya Ethiopia imeweka mabango ya kuwaaibisha wateja ambayo inasema hawajarudisha pesa walizopata wakati wa hitilafu ya kiufundi.

•Benki hiyo inasema imepata karibu robo tatu ya $14m (£12m) ilizopoteza, mkuu wake alisema wiki iliyopita.

Image: BBC

Benki ya Ethiopia imeweka mabango ya kuwaaibisha wateja ambayo inasema hawajarudisha pesa walizopata wakati wa hitilafu ya kiufundi.

Notisi zenye majina na picha zao zilionekana nje ya matawi ya Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE) siku ya Ijumaa.

Benki hiyo inasema imepata karibu robo tatu ya $14m (£12m) ilizopoteza, mkuu wake alisema wiki iliyopita.

Alionya kuwa wanaotunza pesa ambazo si zao watakamatwa.

Mwezi uliopita, hitilafu iliyodumu kwa saa moja iliruhusu wateja katika CBE, benki kubwa zaidi ya kibiashara ya Ethiopia, kutoa au kuhamisha zaidi ya walichokuwa nacho kwenye akaunti zao.

Nje ya tawi la CBE katika mji mkuu, Addis Ababa, bango linaloonyesha picha za watu 28 linasomeka: "Wale ambao hawakurudisha pesa walizochukua isivyofaa kutoka Benki ya Biashara ya Ethiopia."

Vitambulisho vya wanaodaiwa kuwa na fedha hizo pia vinaoneshwa kwenye tovuti ya benki hiyo, zikiambatana na namba za akaunti zao za benki.

CBE ilipakia picha hizo kwenye tovuti yake katika orodha nne, ambazo zilikusanywa kulingana na kiasi cha pesa ambacho wateja walidaiwa kuchukua.

Orodha ya kwanza kuchapishwa ilikuwa ya wateja wanaosemekana kuchukua kati ya $1,890 (£1,500) na $5,300 (£4,200).