Tusidanganyane kwa ground ni kubaya, ni wezi na wadanganyifu-Musalia Mudavadi

Musalia Mudavadi
Image: Ezekiel Aming'a

Kiongozi wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ameikashifu serikali kuhusu kuongezeka kwa deni la Kenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa azma yake ya urais katika eneo la Bomas of Kenya siku ya Jumapili, Mudavadi alisema Kenya imefilisika na iko katika hali mbaya kiuchumi kwa sababu ya madeni mabaya na 'wezi'.

"Tunawezaje kujivunia kuwa serikali imejifilisi wenyewe na wananchi. Tutakubali vipi kuishi kwa kupiga magoti

Kenya iko kwenye njia panda hatari. Serikali inamkaba bukini anayetaga yai la dhahabu,tusidanganyike kwa ground mambo ni mabaya."

HUku akizungumzia kuzindua uchumi wa taifa iwapo atachaguliwa kuwa rais Musalia alisema kuwa;

"Ata hustlers wanahitaji uchumi bora," Musalia alisema huku ukumbi ukipiga mbwembwe ishara ya kuonyesha kwamba wanamuunga mkono.

Mudavadi alisema nchi kwa sasa ni mateka wa majambazi.

"Wanaopaswa kujali wamejikita katika kujilinda kisiasa, na ufisadi mkubwa serikalini. Tusipotengeneza ajira kwa vijana na kuzalisha mali, nchi yetu italipuka," alisema.