Uhuru atakuwa mshauri wangu nitakapokuwa Rais-Raila

Muhtasari
  • Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema zaidi kwamba kuna chaguo nyingi kwa Rais Kenyatta katika serikali yake, ikiwa ni pamoja na "biashara na masuala ya kidiplomasia"
Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga anasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta atakuwa "mshauri" katika serikali yake iwapo atashinda urais Agosti.

 Odinga, katika mahojiano ya Jumanne na mwandishi wa BBC Sophie Ikenye, alisema kuwa rais Kenyatta atakuwa mtu wa kushauriwa, na kuongeza kuwa Rais pia anashauriana naye.

“Atanisaidia kwa ushauri. Nitakuwa nikishauriana naye jinsi anavyonishauri sasa,”Alisema  Odinga.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema zaidi kwamba kuna chaguo nyingi kwa Rais Kenyatta katika serikali yake, ikiwa ni pamoja na "biashara na masuala ya kidiplomasia".

"Anaweza kushughulikia biashara na masuala ya kidiplomasia, jinsi ninavyohudumu katika Umoja wa Afrika, na mengine mengi. Kuna nyadhifa nyingi ambazo Rais Kenyatta anaweza kuhudumu,” aliongeza.

Huku akipongeza urithi wa Rais Kenyatta, Odinga alisema kuwa serikali yake itachukua kutoka kwa miradi ya miundombinu ambayo Kenyatta ataondoka na kuipanua zaidi.

"Uhuru Kenyatta amefanya mambo mengi ya busara ya miundombinu, lakini yote hayo ni kama maji katika bahari, tutaendelea kupanua mtandao wa barabara na umeme kote nchini ili kukuza uchumi," Odinga alisema.