"Muda hauwezi kufuta uwepo wake katika maisha yetu!" Sonko amkumbuka marehemu babake kihisia

Marehemu Gideon Kioko Kivanguli alifariki mnamo Septemba 6, 2015.

Muhtasari

•Marehemu Gideon Kioko Kivanguli alifariki mnamo Septemba 6, 2015 katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

•Mwanasiasa huyo alimkumbuka babake kama mtu mwenye upendo, aliyejitolea, mkarimu, mwenye hekima na mkarimu.

Image: FACEBOOK// MIKE SONKO

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Gideon Mbuvi Kioko almaarufu Mike Sonko ameadhimisha miaka saba tangu kifo cha babake.

Marehemu Gideon Kioko Kivanguli alifariki mnamo Septemba 6, 2015 katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mfupi. Alifariki akiwa na umri wa miaka 67.

Katika chapisho la kumbukumbu ya kifo kwenye Facebook, Sonko alibainisha kuwa kifo cha babake miaka kadhaa iliyopita hakikumaanisha mwisho wa uhusiano wao naye.

"Yani karibu nisahau kuwa leo ni miaka 7 kamili tangu marehemu Baba yangu ateleze kimya kimya hadi milele. Muda ulisimama lakini hauwezi kamwe kufuta uwepo wake katika maisha yetu. Kifo kinaweza kumaliza maisha lakini sio uhusiano," aliandika.

Mwanasiasa huyo alimkumbuka babake kama mtu mwenye upendo, aliyejitolea, mkarimu, mwenye hekima na mkarimu.

"Tunakukumbuka kama zawadi nzuri kutoka kwa Mungu, nguzo yetu ya nguvu. Tunathamini sana kumbukumbu zako za upendo wako, kujitolea, wema, hekima na ukarimu wako ambao utabaki kuwa mwanga wa mwongozo kwetu," alisema.

Aliongeza, "Ingawa uliondoka kimwili, umekuwa wazo lililo mbali nasi kila wakati," 

Mkewe Sonko Primrose Mbuvi pia alimkumbuka baba mkwe huyo wake na kumtakia mapumziko ya amani.

Saumu Mbuvi, bintiye Sonko  pia alizamia kwenye Instagram kumkumbuka marehemu babu yake.

"Endelea kupumzika kwa amani ya milele babu. Tunakumiss," aliandika Saumu.

Kwa sasa Sonko ni yatima kwani pia  alimpoteza mamake Saumu Mukami Mbuvi takriban miaka ishirini na tano iliyopita.

FACEBOOK// MIKE SONKO
Image: Marehemu Gideon Kioko Kivanguli