Jeshi la Uganda litaleta shida-Mike Sonko

Jenerali katika nukuu moja aliuliza kwa kejeli ni wapi Wakenya wanafikiri anapaswa kuishi baada ya uvamizi huo.

Muhtasari
  • Museveni mnamo Jumanne alimpandisha cheo Muhoozi hadi cheo cha Jenerali Kamili kutoka kile cha Luteni Jenerali
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kupitia ukurasa wake wa facebook ametoa maoni yake kuhusu kupandishwa cheo kwa mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba, hadi cheo cha jenerali.

Alidai kuwa hatua hiyo huenda ikafungua milango ya machafuko nchini ambayo yataanza jeshini.

"Hii Uganda haitaenda poa. ngoja muone hivi karibunikutakuwa na shida na hiyo shida italetwa na jeshi. Nakomea hapo kwa sasa," alisemaJumanne.

Museveni mnamo Jumanne alimpandisha cheo Muhoozi hadi cheo cha Jenerali Kamili kutoka kile cha Luteni Jenerali.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, atarithiwa na aliyekuwa Meja Jenerali Kayanja Muhanga, ambaye atachukua nafasi ya kamandi ya majeshi ya nchi kavu.

Kupandishwa cheo kulijiri siku moja baada ya jumbe zenye utata kuhusu kuchukua udhibiti wa Kenya na Nairobi.

Jenerali katika nukuu moja aliuliza kwa kejeli ni wapi Wakenya wanafikiri anapaswa kuishi baada ya uvamizi huo.

"Nina furaha kwamba wanachama wa wilaya yetu nchini Kenya, wamejibu kwa shauku kwenye tweet yangu. Bado ni wiki 2 hadi Nairobi! Baada ya jeshi letu kuteka Nairobi, niishi wapi? Westlands? Riverside?" alisema.