Nataka nisahau machungu ya kuwa na kesi nyingi,'Linturi aambia kamati ya bunge

“Mheshimiwa Mwenyekiti, thamani yangu ya kifedha inajumuisha uwekezaji wangu katika kampuni mbalimbali

Muhtasari
  • Alibainisha kwa sasa ana kesi 35 za madai na hakuna kesi ya jinai mahakamani
  • Aidha waziri huyo amesema kwamba ana thamani ya bilioni 1.2
MITHIKA LINTURI
Image: EZEKIEL AMING'A

Akiwa kwenye mahojiano mbele ya kamati ya bunge waziri mteule wa wizara ya kilimo Mithika Linturi, amesema kwamba anataka kusahau uchungu wa kuwa na kesi nyingi kortini.

Kulingana na Linturi amechoka kupigana na kesi mahakamani, na hana nguvu ya kupigana tena.

Seneta huyo wa zamani, ameacha yote kwa dhamiri za wanaomshtaki na Mungu.

“Nimepigana kesi nyingi sana na nadhani sina nguvu, nataka niikomboe akili nikipewa nafasi ya kufanya kazi kwa ajili ya nchi hii lazima pia niiache, nisahau machungu na mateso niliyopitia. wameziachia dhamiri zao na Mungu awashughulikie kwa sababu ni wengi,” Linturi alisema.

Alibainisha kwa sasa ana kesi 35 za madai na hakuna kesi ya jinai mahakamani.

Aidha waziri huyo amesema kwamba ana thamani ya bilioni 1.2.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, thamani yangu ya kifedha inayojumuisha uwekezaji wangu katika kampuni mbalimbali nchini na uwekezaji mwingine kwenye saccos unafikia Sh1.2 bilioni

"Mapato yangu ya sasa ni pesa ninazopata kutokana na mapato ya kukodisha. Biashara, mimi ni mfugaji wa ng'ombe wa maziwa, na kiasi ninachotarajia kupata siku za usoni ni zaidi ya Sh1 bilioni,"Linturi aliweka wazi.