Kadhaa wahofiwa kukwama ndani ya jengo la ghorofa 7 lililoporomoka Kasarani

Jengo hilo la ghorofa saba lilikuwa likijengwa wakati liliporomoka mwendo wa saa 2.30 mchana, kwa mujibu wa walioshuhudia.

Muhtasari

• Wengi wa wanaohofiwa kunaswa kwenye vifusi ni wajenzi.

• Jengo hilo la ghorofa saba lilikuwa likijengwa wakati liliporomoka mwendo wa saa 2.30 mchana, kwa mujibu wa walioshuhudia.

Jengo la ghorofa 7 laporomoka eneo la Kasarani
Jengo la ghorofa 7 laporomoka eneo la Kasarani

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya jengo kuporomoka eneo la Seasons, Kasarani Jumanne mnamo Novemba 14

Wengi wa wanaohofiwa kunaswa kwenye vifusi ni wafanyikazi wa ujenzi.

Jengo hilo la orofa saba lilikuwa likijengwa wakati liliporomoka mwendo wa saa 2.30 mchana, kulingana na walioshuhudia.

Shughuli za uokoaji zimeanza mara moja huku mashirika ya uokoaji kutoka kaunti ya Nairobi yakifika pale.